MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Vyuo vya Kilimo vishirikishwe mradi wa BBT
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Vyuo vya Kilimo vishirikishwe mradi wa BBT
Habari

Vyuo vya Kilimo vishirikishwe mradi wa BBT

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango amesisitiza ushirikishwaji wa vyuo vya kilimo katika mradi wa Kilimo wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT) ili wanafunzi waweze kujifunza kwa vitendo kilimo cha kisasa.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akiweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Mradi BBT wa Skimu ya Umwagiliaji ya Dkt. Samia Suluhu Hassan – Mlazo/ Ndogowe wakati akiwa ziarani mkoani Dodoma.

Amesema ni muhimu kuondoa dhana ya kwamba kilimo hakina faida kuanzia kwa walimu pamoja na wanafunzi wa kilimo kwa kuwashirikisha katika miradi ya kilimo cha kisasa ikiwemo skimu za umwagiliaji.

Amewasihi wanafunzi wa Vyuo vya Kilimo kutumia muda wa likizo katika kushiriki kwenye miradi hiyo.

Makamu wa Rais amesema Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Dkt. Samia Suluhu Hassan – Mlazo/ Ndogowe ni mradi muhimu kwa Mkoa wa Dodoma ambao una hazina kubwa ya maji chini ya ardhi.

Amesema mradi huo ni suluhisho la kuondokana na tatizo la ukosefu wa chakula cha kutosha

Amewapongeza viongozi na wananchi wa vijiji vya Mlazo na ndogowe kwa kutambua umuhimu wa mradi huo na kutoa ardhi hekari elfu 11 zinazotumika kutekeleza mradi.

Makamu wa Rais amesema Mradi huo utaenda pamoja na ujenzi wa kituo cha afya ili kuwaondolea adha wananchi wa Kijiji cha Mlazo ya kufuata huduma za afya maeneo ya mbali.

Aidha ameagiza kufikishwa kwa huduma ya mawasiliano ya simu katika vijiji hivyo.

Pia Makamu wa Rais ameigiza ya Maliasili na utalii kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Chamwino kuhakikisha inapatikana njia ya Wanyama (usharoba) ili kuwaruhusu Wanyama hao waweze kupita.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amesema katika kuendeleza mradi wa Jenga Kesho Iliyobora katika Kilimo, tayari Wizara imetoa maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya kilimo ambayo yatawekewa miundombinu ya umwagiliaji na kuwawezesha wananchi katika maeneo hayo kuweza kushiriki katika kilimo.

Ameongeza kwamba katika kutoa fursa kwa wananchi wanaoishi katika vijiji vya Mlazo na Ndogowe unakotekelezwa mradi huo, jumla ya hekari 1000 zimetengwa na zitawekwa miundombinu ya umwagiliaji kwaajili ya wanakijiji ambao wataweza kufanya shughuli za kilimo kwa manufaa yao.

Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Dkt. Samia Suluhu Hassan – Mlazo/ Ndogowe
unatekelezwa katika Kijiji cha Mlazo Jimbo la Mvumi Wilayani Chamwino ukigharimu sh bilioni 20.6

Jumla ya vijana 420 kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania watashiriki katika Mradi huo ambapo vijana 50 ni kutoka vijiji vya Mlazo na Ndogowe.

You Might Also Like

Bodi Ya Wadhamini Ya NSSF Yaridhishwa Na Uwekezaji Wa Ubia Na Jeshi La Magereza

Watafiti Wa Mimea Vamizi Watua Serengeti

Mpango Asema Tanzania, Korea Kubadilishana Wafanyakazi

Kagera, Geita kuanza uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura

Madereva Mabasi YA Kukodi Waitwa LATRA Kabla YA Januari 12, Mwaka Huu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TMA yatoa mwelekeo mvua za vuli 2024
Next Article Biashara kidijitali inawezekana soko huru la Afrika
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?