MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TASAC yajipanga kuhudumia wafanyabiashara
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TASAC yajipanga kuhudumia wafanyabiashara
Habari

TASAC yajipanga kuhudumia wafanyabiashara

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limejipanga kutatua changamoto za wadau wanaotumia usafiri wa njia ya maji wanaosafirisha mizigo baina ya Tanzania na Visiwa vya Comoro.
Akitoa salamu za Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Kaimu Meneja wa Usajili na Ukaguzi wa Meli, Said Kaheneko katika Kliniki ya Diaspora nchini Comoro iliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania  amesema ushiriki wa TASAC utaleta matokeo chanya.
Matokeo chanya hayo ni  kwa kuwa wadau wa sekta ya usafiri majini watapata fursa ya kuelezea changangoto zao na wawakilishi wa TASAC waliopo Comoro wataweza kukusanya na kutatua changamoto hizo ambazo zimewasilishwa.
“Timu ya watumishi wa TASAC kutoka Idara mbalimbali wanashiriki  katika Kliniki na hii itakuwa ni fursa nzuri ya kuona namna ya kutatua changamoto za wadau wetu, kutoa elimu kuhusu masuala ya usalama wa vyombo, kutembelea bandari pamoja na kubadilishana Mawazo na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Majini ya hapa Comoro,” amesema.
Aidha amempongeza Balozi wa Tanzania nchini Comoro Saidi Yakubu kwa kuona umuhimu wa kuandaa Kliniki hiyo ambayo imejumuisha wadau mbalimbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi kuweza kukutana na kutatua changamoto zinazowakabilia diaspora pamoja na kuangalia fursa zilizopo katika nchi ya Comoro.
Naye Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu amewashukuru Wakuu wa Taasisi wote walioruhusu maofisa wao kushiriki katika Kliniki ya Diaspora na kutoa rai kwa Diaspora kutumia siku hizo tatu kuweza kufika katika Kliniki ili kuweza kupata huduma.
“Shukrani za kipekee naomba nizipeleke kwa  wakuu wote wa Taasisi zilizofika hapa, kwa kuitikia wito na kukubali kutoa huduma kwa watanzania wanaoishi Comoro.
 “Naamini ujio huu utasaidia wao kupata huduma na changamoto zao kutatuliwa kwa wakati” amesema.
Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro umeaandaa Kliniki hii maalum kwa Diaspora katika viwanja vya Bunge, Moroni kuanzia Agosti tatu hadi sita, 2024 ambapo jumla ya Taasisi 17 zinashiriki na kutoa huduma katika Kliniki hiyo.

You Might Also Like

TUGHE: Wafanyakazi wapewe haki ya kujiunga vyama vya wafanyakazi

VETA Kihonda Waja Na Mashine Ya Kusaga Chumvi Sabasaba

JMAT Yatoa Neno Yanayoendelea Kwa Vijana Wa Kenya

GST Yaelezea Mafanikio Yake

Vyama Vya Wafanyakazi Himizeni Na Kufundisha  Amani Ya Nchi Kuelekea Uchaguzi Mkuu -Ridhiwan

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tume ya umwagiliaji yapambana kuinua kilimo
Next Article UDOM yashauri matumizi ya green house kupata tija
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?