MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tunashauri Ufugaji wa Samaki Kwenye Vizimba, Mavuno ni Mengi – TAFIRI
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tunashauri Ufugaji wa Samaki Kwenye Vizimba, Mavuno ni Mengi – TAFIRI
Habari

Tunashauri Ufugaji wa Samaki Kwenye Vizimba, Mavuno ni Mengi – TAFIRI

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

MTAFITI Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) jijini Mwanza, Philemon Nsinda, amesema kuwa kutokana na upungufu wa samaki unaoendelea kujitokeza katika siku za karibuni, taasisi hiyo imefanya tafiti za kubaini maeneo yanayofaa kwa ajili ya ufugaji wa samaki katika Ziwa Victoria.

Nsinda amesema hayo alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa habari kwenye Maonesho ya Ziwa Victoria yanayoendelea jijini Mwanza.

Amesema maeneo yaliyobainishwa yamewasilishwa serikalini ili yaweze kutengwa na kugawiwa kwa wafugaji wa samaki wenye mahitaji ya kuendesha shughuli hizo.

“Katika siku za karibuni kumekuwa na upungufu wa samaki, hali ambayo imeongeza umuhimu wa kufuga samaki kwenye vizimba.

“Awali watu walifuga kwenye mabwawa, lakini sasa tunawashauri wafuge kwenye vizimba kwa sababu mavuno yake ni makubwa zaidi,” amesema Nsinda.

Aidha, ameeleza kuwa TAFIRI imekuwa ikiendesha tafiti mbalimbali zinazohusiana na uvuvi ili kubaini idadi ya samaki waliopo ziwani kwa kutumia mbinu za kisasa za kitaalamu, ikiwemo teknolojia ya mwangwi, inayosaidia kutoa makadirio ya samaki waliopo ndani ya ziwa.

Pia taasisi hiyo hufanya tafiti za kubaini kiwango cha samaki wanaovuliwa kutoka ziwani ili kupata takwimu sahihi za uzalishaji wa samaki.

Kwa upande wa baiolojia na mazingira, Nsinda amesema watafiti huangalia hali ya maji pamoja na kiwango cha uchafuzi wa mazingira kwa kuchunguza viashiria mbalimbali vinavyopatikana majini.

“Samaki wanahitaji mazingira mazuri ili waweze kuishi na kuzaliana vizuri. Maji yanapochafuka, uzalishaji wa samaki hupungua kwa kiwango kikubwa,” amesema.

Vilevile, amesema taasisi hiyo hufanya tafiti za sayansi jamii zinazolenga kuwafahamu watu wanaotumia samaki kama sehemu ya lishe yao pamoja na wale wanaotaka kujihusisha na shughuli za uvuvi.

Ameongeza kuwa tafiti hizo husaidia kubaini mahitaji ya jamii na kutoa mwongozo sahihi kuhusu maendeleo ya sekta ya uvuvi nchini.

Nsinda amesema Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) ina vituo vikubwa vinne vya utafiti, vikiwemo vya Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria pamoja na kituo cha baharini cha Kunduchi kilichopo Dar es Salaam.

You Might Also Like

Serikali Imetoa Ruzuku Ya Asilimia 20 Hadi 50 Kwenye Mitungi YA Gesi – Kapinga

TPHPA Yapata Dawa Ya Visumbufu Vya Mazao

Nyamhokya: Mei Mosi Ni Singida Mwaka Huu 2025

Ridhiwani, Waziri Wa Kazi, Ajira UAE Waweka mkakati

Mashimba: Tumieni Siku Zilizobaki Kujiandikisha

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Utafiti wa Chakula Bora cha Kuku wa Nyama Watoa Tumaini kwa Wafugaji
Next Article Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Yasisitiza Uhifadhi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Yasisitiza Uhifadhi
Habari May 20, 2026
Utafiti wa Chakula Bora cha Kuku wa Nyama Watoa Tumaini kwa Wafugaji
Makala May 19, 2026
JWTZ Kulipa Fidia Wananchi Waliochukuliwa Maeneo
Habari May 19, 2026
Timu Ya Bunge Yakabidhiwa Vifaa Vya Michezo
Habari May 19, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?