MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ikomba: Acheni Makundi, Jengeni Umoja wa Chama
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ikomba: Acheni Makundi, Jengeni Umoja wa Chama
Habari

Ikomba: Acheni Makundi, Jengeni Umoja wa Chama

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: RAIS wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Dkt. Suleiman Ikomba, amewaonya walimu na watumishi wa chama hicho kuacha tabia ya uchonganishi na kueneza taarifa zisizo na msingi, akisema mwenendo huo unadhoofisha utendaji na mshikamano ndani ya taasisi.
Dkt. Ikomba ametoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na Kamati ya Utendaji ya Taifa ya CWT pamoja na watumishi wa Makao Makuu ya chama katika kikao kilichofanyika St. Gaspar, jijini Dodoma.
Amesema CWT ina dhamana kubwa kwa walimu wa Tanzania, hivyo mafanikio yake hayategemei viongozi waliochaguliwa pekee, bali pia juhudi, uadilifu na ushirikiano wa watumishi wake.
Amekiri kuwepo kwa changamoto za kiutumishi katika Makao Makuu ya chama, zikiwemo migogoro, kutokuelewana, kupungua kwa ushirikiano baina ya idara na tabia ya uchonganishi, hali inayosababisha baadhi ya watumishi kufanya kazi kwa mashaka.
“Ni lazima tukubaliane kuwa mazingira ya aina hii hayawezi kusaidia taasisi kusonga mbele kwa ufanisi tunaoutarajia,” amesema.
Amesisitiza umuhimu wa kuheshimu majukumu na mamlaka ya kila nafasi ndani ya chama, akieleza kuwa ingawa viongozi huchaguliwa kwa vipindi maalum, taasisi yenyewe ni ya kudumu na inahitaji utamaduni wa kuheshimiana.
Aidha, amewataka watumishi kufanya kazi kwa misingi ya taaluma, uadilifu na kuepuka upendeleo, huku akionya kuwa kujihusisha na makundi au kampeni za uchaguzi wa ndani huacha athari hasi katika utendaji baada ya uchaguzi.
“Tunachohitaji ni utamaduni wa kuweka mbele maslahi ya chama na wanachama wake badala ya makundi au maslahi binafsi,” amesisitiza.
Ameeleza matarajio ya uongozi kuwa kila idara itekeleze majukumu yake kwa kuzingatia mipango kazi, kuimarisha ushirikiano miongoni mwa watumishi, na kuheshimu taratibu za kiutumishi.
Dkt. Ikomba amesema ana imani kuwa watumishi wanaweza kurekebisha hali iliyopo na kujenga upya mazingira bora ya kazi, akisisitiza kuwa Makao Makuu yanapaswa kuwa mfano wa nidhamu, weledi na mshikamano kwa wanachama kote nchini.
Amewataka watumishi kuanza ukurasa mpya kwa kufanya kazi kwa pamoja, kuheshimiana na kuweka mbele maslahi ya chama, akibainisha kuwa taasisi yoyote inayotaka kufanikiwa lazima ijengwe juu ya misingi ya nidhamu, uwajibikaji na uadilifu.
Ameongeza kuwa uongozi utaendelea kusimamia kwa karibu utendaji wa kazi ili kuhakikisha kila mtumishi anatimiza wajibu wake ipasavyo.
“Ni matumaini yangu kuwa tutafanya kazi kwa mshikamano na kuweka mbele maslahi ya chama. Tukisimama pamoja, CWT itaendelea kuwa imara na yenye heshima kwa walimu na taifa kwa ujumla,” amesema.

You Might Also Like

Maboresho sheria, kanuni za madini yameongeza mapato

Mabalozi Wa Utalii Waahidi Kuulinda Ushoroba Wa Kwakuchinja

Ongezeni Uwajibikaji,Nidhamu, Utendaji Kazi – Bashungwa

VETA Dodoma Waleta Mashine Kurahisishia Upekechuaji Wa Alzeti

‎NIRC Imechimba Visima 362, , Yahamasiha Wakulima Kunufaika Na Program Ya Umwagiliaji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yaimarisha Vitengo vya Tathmini na Ufuatiliaji Kuwa Huduma Bora kwa Wananchi
Next Article Mbunge Ndoinyo Aitaka Serikali Kugawa Ngorongoro Kusogeza Huduma Karibu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TPHPA yawataka wakulima, wafanyabiashara kulinda ubora wa mazao, yafungua soko la viazi Zambia
Habari August 27, 2026
PBPA Yashiriki Tamasha La Nne La Kitaifa La Utamaduni
Habari August 27, 2026
TFNC Yahimiza Wanaotoa Ushauri Wa Lishe Mitandaoni Kushirikiana Na Taasisi Zenye Mamlaka
Habari August 27, 2026
TaSUBa Yahimiza Vijana Kuzifikia Fursa Za Mafunzo Ya Sanàa Na Utamaduni
Habari August 27, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?