MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Rais Dkt Samia Kuzindua Miradi Katika Mji Wa Serikali Mtumba,Dodoma
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Rais Dkt Samia Kuzindua Miradi Katika Mji Wa Serikali Mtumba,Dodoma
Habari

Rais Dkt Samia Kuzindua Miradi Katika Mji Wa Serikali Mtumba,Dodoma

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu -Dodoma
RAIS  Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua majengo ya Ofisi za Wizara, Taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 57.1 katika Mji wa Serikali Mtumba,Jijini Dodoma.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika jumanne Septemba  8,2026 katika Uwanja wa Mashujaa uliopo ndani ya Mji wa Serikali Mtumba.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba Kabudi, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya hafla hiyo.
Habari Picha 13639
Amesema uzinduzi huo utahusisha maeneo matatu makuu ambayo ni majengo ya Ofisi za Wizara 26, Taasisi 11 za Serikali na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 57.1.
Profesa Kabudi amesema kukamilika kwa majengo hayo, kutawezesha watumishi 18,510 kutumia ofisi za Mji wa Serikali, Mtumba.
“Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba ulianza kutekelezwa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa majengo 23 ya Ofisi za muda.ujenzi wa majengo hayo ulianza Novemba 28 mwaka  2018 na kukamilika Machi 22 mwaka 2019, hatua iliyowezesha baadhi ya watumishi wa Wizara na taasisi kuanza kuhamia.
Ameongeza kuwa :” Awamu ya pili ya ujenzi ilianza Oktoba, 2021, ikiwa inalenga kujenga majengo ya kudumu kwa ajili ya watumishi wote wa Wizara na Taasisi zilizopangwa kuhamia Mtumba.Pia ilihusisha ujenzi wa miundombinu na huduma mbalimbali za kijamii, ikiwemo barabara za lami.
Habari Picha 13640
Profesa Kabudi amesema mbali na barabara hizo, miundombinu ya kudumu ya mawasiliano pamoja na Uwanja wa Mashujaa imekamilika na itakuwa sehemu ya miundombinu itakayotumika katika shughuli za Serikali.
Hata hivyo, amesema baadhi ya miradi bado iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya umeme inayopita chini ya ardhi yenye urefu wa kilomita 42.
“Kazi ya ujenzi wa miundombinu ya maji safi na uondoshaji wa maji taka, TEHAMA, ufungaji wa mifumo ya usalama ya CCTV Camera, ujenzi wa kituo cha zimamoto pamoja na utekelezaji wa mpango wa upandaji miti na ustawishaji wa Mji wa Serikali nazo zinafanyika, “amesema.
Habari Picha 13641
Amesema Rais Dkt.Samia ameendelea kuweka msisitizo katika kuboresha mazingira hayo, ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa samani za Wizara na taasisi 26 zinazohamia katika majengo hayo.
Profesa Kabudi amesema hatua hizo zinaendelea kuifanya Mji wa Serikali Mtumba kuwa miongoni mwa alama muhimu za utekelezaji wa dhana ya Dodoma kuwa kitovu cha shughuli za Serikali.
Amesema uwekezaji huo pia unatarajiwa kuongeza fursa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla.
Habari Picha 13642
Habari Picha 13643

You Might Also Like

SUA Chatumia Ngamia Mafunzo Ya Vitendo Kwa Wanafunzi

TADB Yapongezwa Kwa Kuuongeza Uzalishaji Wa Mazao Nchini,Kuinua Kipato

TUCTA: Waajiri Watekeeze Nyongeza Ya Kima cha Mishahara Sekta Binafsi

Ukosefu wa Chakula Shuleni Waathiri Wanafunzi Longido, CORDS Waja na Mrad

Majaliwa awasili Kilimanjaro kufungua semina Mambo ya Ndani

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mradi Wa Umeme Mpomvu-GGM Kuimarisha Upatikanaji Wa Umeme Na Kuchochea Shughuli Za Kiuchumi Geita- Salome
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mradi Wa Umeme Mpomvu-GGM Kuimarisha Upatikanaji Wa Umeme Na Kuchochea Shughuli Za Kiuchumi Geita- Salome
Habari September 4, 2026
Wahitimu 794 Wa Vyuo Vya Elimu Ya Juu Waomba Kujiunga VETA
Habari September 4, 2026
Taka za saluni zageuka dhahabu ya kijani: COSTECH yamulika safari ya David kutoka wazo hadi hataza
Makala September 4, 2026
Umeme Kubadilisha Maisha Ya Wakazi Wa Kisiwa Cha Jibondo Mafia
Habari September 3, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?