MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mradi Wa Umeme Mpomvu-GGM Kuimarisha Upatikanaji Wa Umeme Na Kuchochea Shughuli Za Kiuchumi Geita- Salome
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mradi Wa Umeme Mpomvu-GGM Kuimarisha Upatikanaji Wa Umeme Na Kuchochea Shughuli Za Kiuchumi Geita- Salome
Habari

Mradi Wa Umeme Mpomvu-GGM Kuimarisha Upatikanaji Wa Umeme Na Kuchochea Shughuli Za Kiuchumi Geita- Salome

Author
By Author
Share
4 Min Read

 

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inaendelea kuimarisha miundombinu ya umeme nchini kupitia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Mpomvu hadi kituo cha kupokea na kupoza umeme cha GGM, wenye urefu wa takribani kilomita 6.7.
Akizungumza Septemba jijini Dodoma, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema kukamilika kwa mradi huo kutaimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuchochea shughuli za kiuchumi, ikiwemo uzalishaji, ajira, ongezeko la mapato na uwekezaji.
Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na TANESCO na wadau wa sekta ya nishati kuhakikisha miundombinu ya umeme inaendana na kasi ya ukuaji wa mahitaji.
“Serikali itaendelea kushirikiana na TANESCO na wadau wote wa sekta ya nishati kuhakikisha miundombinu ya umeme inaendana na kasi ya ukuaji wa mahitaji. Tunataka kuona umeme unaozalishwa nchini ukitumika kikamilifu kuchochea uzalishaji, kuongeza ajira, kuongeza mapato na kuvutia uwekezaji zaidi. Mradi huu ni kielelezo cha falsafa hiyo,” amesema Mhe. Salome.
Habari Picha 13628
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,  Lazaro Twange, amesema mradi huo unatekelezwa kwa miezi 18 kutoka tarehe ya utiaji saini mkataba ukilenga kukidhi ongezeko la mahitaji ya umeme kwa GGM.
“Mradi huu unagharimu takribani Sh bilioni 63.19 za Kitanzania na kutokana na kuwa GGM ni miongoni mwa wateja wetu wakubwa wenye kuchangia kiasi kikubwa cha mapato kwa Shirika, tutahakikisha mradi huu unafanikiwa kama inavyotarajiwa kukidhi ongezeko la mahitaji yao kwa manufaa ya pande zote mbili na pato la Taifa kwa ujumla,” amesema  Twange.
Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Balozi Zuhura Bundala, amesema utiaji saini wa mkataba huo ni sehemu ya hatua za kimkakati za kujenga uwezo wa TANESCO kukidhi mahitaji ya wateja na kufungua fursa za uwekezaji na ajira.
Habari Picha 13629
“Utiaji saini huu ni sehemu ya kimkakati kujenga uwezo wa TANESCO kukidhi mahitaji ya wateja na kufungua fursa za uwekezaji na ajira. Bodi tutaendelea kuisimamia TANESCO kukidhi ongezeko la hitaji la umeme kwa kuimarisha na kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu ya umeme,” amesema  Bundala.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini,  Subira Mgalu, ameipongeza Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO kwa namna inavyosimamia Shirika katika ujenzi wa uchumi wa kisasa kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
“Niipongeze Bodi ya Wakurugenzi TANESCO kwa namna mnavyosimamia Shirika hili kujenga uchumi wa kisasa kuelekea Dira 2050. Utekelezaji wa mradi huu unatupa nguvu zaidi kwa sababu sekta zote, nishati na madini, zipo chini yetu,” amesema Mhe. Mgalu.
Habari Picha 13630
Naye Mkuu wa Wilaya ya Geita,  Hashimu Komba, akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo amesema Uongozi wa Mkoa umejipanga kushirikiana na mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha utekelezaji wake haupati kikwazo, akisisitiza umuhimu wa nishati ya umeme katika kuchochea maendeleo ya sekta mbalimbali.
“Ni dhahiri, nishati ya umeme inachagiza maendeleo ya sekta zote. Tunampongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anavyosukuma kwa dhati agenda ya nishati ya umeme kuwafikia wananchi. Mamlaka ya Mkoa imejipanga kushirikiana na Mkandarasi wa mradi wa umeme wa Mpomvu–GGM kuhakikisha mradi haupati kikwazo,” amesisitiza  Komba.
Habari Picha 13631
Habari Picha 13632
Kukamilika kwa mradi huo, kutatoa fursa ya njia ya awali ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoto 33 iliyokuwa ikipelekea umeme GGM,  kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika Mkoa wa Geita na maeneo ya pembezoni , vilevile kuwezesha wananchi kuendesha shughuli zao za uzalishaji kwa ufanisi, pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa uwekezaji mpya ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha  na kuongeza uwezo wa mfumo wa usafirishaji na usambazaji wa umeme kukidhi mahitaji ya sasa na
yajayo.

 

 

You Might Also Like

Shule 216 Za Serikali Zatumia Nishati Safi Ya Kupikia – Kapinga

Wizara Ya Madini Kununua Chopa, Kufanya Utafiti

Kamishna TRA Atua Kwa Malasusa Kushirikiana Elimu Kwa Mlipa Kodi

Vijana Watakiwa Kuanza Utekelezaji Wa Mipango Waliyonayo

Kadi za mpiga kura zenye jina la zamani la Tume ni halali

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wahitimu 794 Wa Vyuo Vya Elimu Ya Juu Waomba Kujiunga VETA
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wahitimu 794 Wa Vyuo Vya Elimu Ya Juu Waomba Kujiunga VETA
Habari September 4, 2026
Taka za saluni zageuka dhahabu ya kijani: COSTECH yamulika safari ya David kutoka wazo hadi hataza
Makala September 4, 2026
Umeme Kubadilisha Maisha Ya Wakazi Wa Kisiwa Cha Jibondo Mafia
Habari September 3, 2026
Tanzania Yalenga Kuzalisha, Si Kununua Teknolojia
Habari September 3, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?