Hananja Awataka Vijana Kufikiri Mara Mbili Kabla ya Kufuata Wito wa Maandamano
Na Lucy Lyatuu,Dodoma
MCHUNGAJI Richard Hananja amewataka vijana kutafakari kwa kina kabla ya kushiriki maandamano au vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani ya nchi, akisisitiza kuwa tofauti za mitazamo zinapaswa kujenga mazungumzo na maelewano, si migawanyiko.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Juni 18, 2026, Hananja ameonya dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yanayoweza kuchochea chuki, matusi na vurugu, huku akiwahimiza vijana kutumia majukwaa hayo kwa uwajibikaji.
Amesema vijana wanapaswa kuwa waangalifu na wito unaotolewa mtandaoni, akibainisha kuwa wengi wa wanaohamasisha maandamano na vurugu hawapo nchini na hawaathiriki moja kwa moja na madhara yake, huku athari kubwa zikiwakumba wananchi waliopo nchini.
[18/06, 6:18 pm] Jane Jumikita: Hananja Aonya: Maandamano Yasivuruge Amani na Umoja wa Taifa.
Mchungaji Richard Hananja amesema changamoto zinazojitokeza katika jamii zinapaswa kutatuliwa kwa mazungumzo na maridhiano badala ya migogoro. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Juni 18, 2026, amesema historia inaonesha kuwa hata uhuru wa Tanzania ulipatikana kupitia mazungumzo.
Hananja amesisitiza kuwa amani ni tunu muhimu inayopaswa kulindwa na kila Mtanzania, akionya kuwa kuvunjika kwake huwaathiri zaidi watoto na wazee. Aidha, ametoa wito wa kutafuta suluhu za tofauti kwa ustaarabu huku akieleza kuwa kujenga amani ni kazi ngumu lakini kuiharibu ni jambo la muda mfupi.
