MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wizara ya Maji: Uhifadhi Ziwa Victoria Unahitaji Ushirikiano, Uwekezaji Endelevu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wizara ya Maji: Uhifadhi Ziwa Victoria Unahitaji Ushirikiano, Uwekezaji Endelevu
Habari

Wizara ya Maji: Uhifadhi Ziwa Victoria Unahitaji Ushirikiano, Uwekezaji Endelevu

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
MWANZA: NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Rose Ambrose, amesema kazi ya uhifadhi na uendelezaji wa Ziwa Victoria inahitaji fedha za kutosha, utangamano pamoja na ushirikiano wa karibu katika ngazi zote, kutokana na ukweli kwamba changamoto za maji duniani zimeongezeka na kuvuka mipaka ya kiutawala.
Rose Ambrose ameyasema hayo wakati akifungua warsha ya wadau wa Bonde la Ziwa Victoria, iliyofanyika jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kwanza ya Ziwa Victoria.
Amesema changamoto hizo ni pamoja na upungufu wa maji, ukame, mafuriko, uchafuzi wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi, hali inayohitaji juhudi za pamoja kati ya mataifa na wadau mbalimbali.
Habari Picha 12153
Kutokana na hali hiyo, amewaalika wadau wa maendeleo kuwekeza katika uhifadhi na usimamizi endelevu wa rasilimali za maji za Ziwa Victoria ili kuhakikisha uhai wake unadumu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Ameeleza kuwa usimamizi wa rasilimali za maji unahitaji mshikamano wa jamii na mataifa, akisisitiza kuwa maji ni kiungo muhimu cha kuunganisha watu.
“Maji yanalazimisha jamii kuungana na kushirikiana,” amesema.
Aidha, ametoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, jumuiya ya kimataifa, washirika wa maendeleo, wataalamu, watafiti, asasi za kiraia na wadau wengine kushiriki kikamilifu katika juhudi za kulinda na kuhifadhi Ziwa Victoria.
Habari Picha 12154
“Kila mmoja akiwa balozi mzuri wa uhifadhi wa Ziwa Victoria kwa kufanya shughuli za kulinda mazingira na kuzuia shughuli hatarishi, tutafanikiwa,” ameongeza.
Warsha hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwa na kaulimbiu isemayo, “Maji Yetu, Mustakabali Wetu, Tuungane kwa Usimamizi Endelevu wa Bonde la Ziwa Victoria’.

You Might Also Like

Kamati YA Siasa Yaendelea Kukagua Miradi Ya Maendeleo Temeke

Kipanga: Lugha ya Kichina Inakuza Diplomasia, Kuimarisha Uhusiano

Tanzania Yapongeza China Kwa Kuimarisha Uhusiano Wa Kidiplomasia Kupitia Lugha, Utamaduni

Tanzania Yaibuka Kidedea Maonesho Zambia

Sheria ya ajira, mahusiano kazini ipitiwe upya

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article MAIPAC NA THRDC Watoa Mafunzo Kwa Waandishi Wa Habari Za Mazingira, Kanda Ya Ziwa
Next Article Wizara Ya  Ujenzi Kutekeleza Vipaumbele Sita,Ujenzi Wa Miundombinu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Uwekezaji wa Vijana Watajwa Chachu ya Ukuaji wa Uchumi
Habari June 29, 2026
Tanzania Yaendelea Kuimarisha Usalama Na Ulinzi Wa Taarifa Binafsi
Habari June 29, 2026
WCF Yapigia Debe Ushirikiano na Teknolojia Kuimarisha Hifadhi ya Jamii
Habari June 28, 2026
Sabasaba 2026 Kuingiza Teknolojia Mpya na Fursa za Uwekezaji
Habari June 27, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?