MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania yaendelea kuwa Shule ya Utumishi Barani Afrika,
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania yaendelea kuwa Shule ya Utumishi Barani Afrika,
Habari

Tanzania yaendelea kuwa Shule ya Utumishi Barani Afrika,

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read

Na Jawadu Kinyobwa

TANZANIA imezidi kujiimarisha kama kitovu cha mafunzo utawala bora barani Afrika baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, kupokea ujumbe wa watu 25 kutoka nchini Somalia kwa ajili ya programu maalumu ya mafunzo ya kuendesha shughuli za utumishi wa umma kwa ufanisi.
Akizungumza mara baada ya kuwakaribisha wajumbe hao Aprili 29 , Ridhiwani ameeleza ujio huo ni kielelezo cha imani ambayo mataifa mengine wanayo kwa Tanzania kama nchi ya mfano katika kuimarisha amani, utulivu na maendeleo ya kiutawala.
Habari Picha 11939
Amesema lengo kuu la ugeni huo ni kujifunza namna mifumo ya utumishi wa umma nchini inavyofanya kazi, ikiwemo usimamizi wa rasilimali watu na namna utumishi huo unavyoweza kujibu kero za wananchi kwa haraka na usahihi.
Waziri Kikwete amesisitiza kuwa Watanzania wapaswa kujua kwamba “wamekalia dhahabu” kutokana na mabadiliko makubwa ya kimfumo yaliyofanyika, hususan katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita inayowezesha wananchi kuwasiliana moja kwa moja na serikali yao.
Amebainisha kuwa matumizi ya teknolojia yamerahisisha huduma ambapo kwa sasa mtumishi wa umma hahitaji kusafiri kutoka mkoani kwenda Dodoma kufuata huduma, bali anaweza kupata mahitaji yake, ikiwemo maombi ya mikopo na mawasiliano na viongozi, kupitia mifumo ya kidijitali iliyowekwa.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Xavier Daudi, amefafanua kuwa wajumbe hao watapitishwa kwenye maeneo muhimu ya kiutendaji ikiwemo muundo wa serikali, mifumo ya Serikali Mtandao na mbinu za kisasa za utunzaji wa nyaraka.
Amesema upekee wa mifumo ya Tanzania na miundombinu yake ya kisasa ya kiutendaji ndivyo vinavyovutia nchi nyingi za Afrika Mashariki na kwingineko kuja kujifunza.
Awali akizungumza Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Ernest Mabonesho, ambaye ndiye mratibu wa programu hiyo, amebainisha kuwa mafunzo hayo ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2025 kupitia Wizara ya Mambo ya Nje.
Amesema zoezi hilo ni muendelezo wa ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Somalia, wenye lengo la kujenga kuwezesha serikali kufanya kazi kwa tija na kwa manufaa ya mataifa yote mawili.
Naye, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Somalia, Ayan Andullahi ameeleza kuwa kupitia mafunzo hayo amejifunza kwa kina kuhusu namna Tanzania ilivyofanikiwa kujenga mifumo madhubuti ya utumishi wa umma inayozingatia uwajibikaji, uwazi na utoaji wa huduma ufanisi na kwa wakati.
Amesisitiza kuwa, uzoefu alioupata, hususan katika matumizi ya mifumo ya kidijitali na uratibu wa rasilimali watu utakuwa chachu ya mageuzi katika taasisi yao pindi watakaporejea nchini Somalia

You Might Also Like

Hananja Awataka Vijana Kufikiri Mara Mbili Kabla ya Kufuata Wito wa Maandamano

Sekta Ya Benki Iko Imara- Gavana BOT

Ufugaji wa sungura ni fursa  – UDOM

Wana Dodoma Wakoshwa Na Uboreshaji Mitaala

Rais Mpya CWT Ikomba: ‘Nataka Kuwaunganisha Walimu, Kuitendea Haki Kazi Yetu’

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wizara Ya Kilimo Yaomba Bunge Kuidhinisha Trilioni 1.1,Yaweka Mikakati Kuimarisha Sekta Hiyo
Next Article Mwandishi Lucy Ngowi Miongoni mwa Waliong’ara Mei Mosi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wadau Wa Kilimo Iondoeni Nchi Kwenye Uchuuzi Wa Mafuta Ya Kula-Chongolo
Habari July 30, 2026
Wadau Wa Kilimo Iondoeni Nchi Kwenye Uchuuzi Wa Mafuta Ya Kula-Chongolo
Habari July 30, 2026
Mradi Wa Njia Ya Kusafirisha Umeme Wa Msongo Wa Kilovolti 400 Chalinze -Dodoma Mbioni Kukamilika
Habari July 29, 2026
Kutoka Wazo Rahisi Hadi Mapinduzi ya Kilimo: Safari ya Rafiki Planter Inayosimulia Miaka 40 ya COSTECH
Makala July 28, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?