MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: ‘Upungufu wa Wakunga Afrika Watishia Maisha ya Mama na Mtoto ‘TAMA
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > ‘Upungufu wa Wakunga Afrika Watishia Maisha ya Mama na Mtoto ‘TAMA
Habari

‘Upungufu wa Wakunga Afrika Watishia Maisha ya Mama na Mtoto ‘TAMA

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu
CHAMA cha Wakunga Tanzania (TAMA) kimetangaza kuadhimisha Siku ya Mkunga Duniani kuanzia Mei 2 hadi 5 mwaka huu mkoani Kilimanjaro, huku kikionya juu ya upungufu mkubwa wa wakunga unaoendelea kuhatarisha maisha ya akina mama na watoto wachanga.
Akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam Leo Rais wa TAMA, Beatrice Mwilike amesema takwimu zinaonesha kuwa bara la Afrika linakabiliwa na upungufu wa takribani wakunga 460,000, hali inayochangia ongezeko la vifo vya mama na mtoto, hasa katika maeneo yenye changamoto za majanga na huduma duni za afya.
Amesema mbali na uhaba huo, vituo vingi vya kutolea huduma za afya vinakumbwa na changamoto za miundombinu na mazingira yasiyo rafiki kwa wakunga, ikiwemo ukosefu wa maji safi, vyoo bora na mazingira salama ya usafi binafsi, hali inayohatarisha usalama wa mama na mtoto wakati wa kujifungua.
“Upungufu wa wakunga si takwimu tu, bali ni maisha ya akina mama na watoto yaliyo hatarini kila siku. Tunahitaji uwekezaji wa haraka, mafunzo zaidi na kuboresha mazingira ya kazi ili kuhakikisha uzazi salama,” amesema Mwilike.
Ameeleza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo “Dunia inahitaji wakunga milioni moja zaidi”, yakilenga kuongeza idadi ya wakunga pamoja na kuimarisha huduma za afya ya uzazi.
Habari Picha 11826
Kwa mujibu wa Mwilike, shughuli zitakazofanyika ni pamoja na mbio za “Mkunga Half Marathon”, maonesho ya huduma za afya kwa jamii, pamoja na mafunzo maalum kwa wakunga ili kuongeza ujuzi na weledi katika taaluma hiyo.
Ameongeza kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa wakunga, kuchochea uwekezaji na sera bora, pamoja na kukusanya rasilimali zitakazosaidia kuboresha huduma za afya ya uzazi nchini.
Kwa upande wake, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Joyce Muna amesema bado kuna upungufu mkubwa wa watoa huduma za afya, jambo linaloathiri utoaji wa huduma bora kwa mama na mtoto.
“Tunatoa wito kwa wauguzi na wakunga kujitokeza kushiriki mbio hizi, kwani ni fursa ya kuchangia upatikanaji wa vifaa tiba vitakavyosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto. Wakunga ni nguzo muhimu ya uzazi salama na ndio wanaompokea mtoto mara ya kwanza anapozaliwa,” amesema Muna.
Naye Mratibu wa Chama cha Wakunga kutoka Canada, Stephano Simba ameipongeza TAMA kwa maandalizi ya maadhimisho hayo, akibainisha kuwa wanaendelea kushirikiana katika miradi ya uzazi salama kwa lengo la kuwajengea uwezo wakunga wanafunzi na wataalamu wa afya.
Amesema ushirikiano huo unalenga kuongeza ujuzi na stadi kwa watoa huduma za afya ili kuboresha huduma na kupunguza vifo vya mama na mtoto, huku akisisitiza umuhimu wa wadau na serikali kuendelea kuwekeza katika sekta hiyo muhimu.

You Might Also Like

Kiwanda cha Sukari Mkulazi Chaanza Kuleta Tija, Sangu Apongeza Uwekezaji wa NSSF na Magereza

Viongozi Watakiwa Kuweka Haki Mbele Katika Kusimamia Masuala ya Wafanyakazi — COWTU (T)

Wiki ya kudhibiti bidhaa bandia kuhitimishwa DSM

Kikwete: Waambieni Tunataka Maendeleo Sio Maneno

Serikali Yazindua Soko Kuu Jipya la Kariakoo Baada ya Moto wa 2021

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kisima Kimoja Cha Gesi Chaonesha Mshangao Kwa Uzalishaji Wa Gesi-PURA
Next Article Mandingo: Jiungeni Mkunga Marathon Kuokoa Maisha ya Mama na Mtoto
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tume Ya Ulinzi Wa Taarifa Binafsi Yatoa Siku Saba Kwa Taasisi Kujisajili
Habari June 12, 2026
Teknolojia Ya Juisi YA Ndizi Kali Yafungua Fursa Mpya Za Viwanda, Ajira
Makala Uncategorized June 12, 2026
Serikali Yaingia Makubaliano Ya Ushirikiano Na DIT Kuimarisha Usimamizi Wa Mataifa
Habari June 8, 2026
Wananchi Waelimishwa Masharti ya Kubadilisha Noti Zilizochakaa, Kuungua na Kuchanika
Habari June 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?