MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yazindua Soko Kuu Jipya la Kariakoo Baada ya Moto wa 2021
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yazindua Soko Kuu Jipya la Kariakoo Baada ya Moto wa 2021
Habari

Serikali Yazindua Soko Kuu Jipya la Kariakoo Baada ya Moto wa 2021

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: RAIS wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Februari 8, 2026 amefungua rasmi Soko Kuu Jipya la Kariakoo jijini Dar es Salaam, akisisitiza kuwa mradi huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha mazingira ya biashara, kuongeza tija ya uchumi na kulinda mitaji ya wafanyabiashara.
Rais Dkt. Samia amesema ujenzi wa soko hilo ni matokeo ya dhamira ya Serikali ya kurejesha Soko la Kariakoo baada ya soko la awali kuteketea kwa moto Julai 2021, kwa kufanya ukarabati na kujenga soko jipya linalokidhi viwango vya usalama, ubora na mahitaji ya biashara ya kisasa.
Amehimiza uendeshaji wa soko hilo kuzingatia misingi ya ufanisi, nidhamu na ushindani wa haki, akibainisha kuwa Kariakoo ni mhimili wa biashara ya kitaifa na kikanda, na kitovu muhimu cha uchumi kinachowaunganisha wazalishaji, wasambazaji, wauzaji na wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi.
Vilevile, Rais Dkt. Samia ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), makandarasi na wasimamizi wa mradi kwa kujenga miundombinu yenye ubora wa hali ya juu, ikiwemo mifumo ya usalama na huduma za kijamii.
Ameuelekeza uongozi wa soko kuendelea kuimarisha mazingira rafiki kwa wanawake wafanyabiashara, ikiwemo huduma za mama na mtoto.
Katika kuhakikisha uendeshaji wenye tija, Rais Dkt. Samia amesisitiza umuhimu wa mifumo thabiti ya zimamoto, uokoaji na dharura, pamoja na upangaji rasmi wa ratiba za kushusha na kupakia mizigo ili kupunguza msongamano na kurahisisha biashara.
Akihitimisha, Rais Dkt. Samia amesema Soko Kuu Jipya la Kariakoo ni uwekezaji wa kimkakati wa Taifa unaopaswa kulindwa na kusimamiwa kwa ufanisi, ili liendelee kuwa injini ya uchumi na mfano wa masoko ya kisasa barani Afrika.

You Might Also Like

OUT Yawapiga Msasa Watumishi Wa Mamlaka Za Serikali Za Mitaa

Nchemba Afungua Mafunzo Ya PAC

ALAT Kujadili Ripoti Ya CAG

Wanataaluma Wahimizwa Kutumia Tafiti Kama Chachu ya Mabadiliko ya Jamii

Waziri Mkuu Majaliwa Akoshwa Na Tafiti Ya Mhitimu OUT

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TALGWU Yaipongeza Timu Ya Makatibu Wa Mikoa Na Mawakili Wa Kanda Kwa Kutoa Huduma Bora Kwa Wanachama
Next Article CWT Yaiomba Serikali Kurekebisha Sheria za Vyama vya Wafanyakazi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Timu Ya Bunge Yakabidhiwa Vifaa Vya Michezo
Habari May 19, 2026
Ndoinyo Aishauri Serikali Kurejesha Utalii Vijijini
Habari May 19, 2026
Nyavu za Plastiki Zatishia Afya za Watumiaji wa Samaki Ziwa Victoria
Habari May 19, 2026
Utunzaji Ziwa Victoria Wasisitizwa kwa Mustakabali wa Uchumi, Mazingira
Habari May 19, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?