MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ofisi ya Rais Mipango Yaomba Bilioni 144.85 kwa Bajeti 2026/27
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ofisi ya Rais Mipango Yaomba Bilioni 144.85 kwa Bajeti 2026/27
Habari

Ofisi ya Rais Mipango Yaomba Bilioni 144.85 kwa Bajeti 2026/27

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amewasilisha rasmi hotuba ya mapendekezo ya bajeti ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27, akieleza mwelekeo wa mapato, matumizi na vipaumbele vya maendeleo.
Akiwasilisha bungeni, Profesa Mkumbo amesema kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina (Fungu 007), Serikali imepanga kukusanya na kuchangia Sh. Trilioni 1.79 katika Mfuko Mkuu wa Serikali kutoka vyanzo visivyo vya kodi.
Vyanzo hivyo ni pamoja na gawio, michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi ya taasisi za umma, mapato ya Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS), riba za mikopo, pamoja na mapato mengineyo.
Kwa upande wa matumizi, amesema Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji pamoja na taasisi zake zinaomba kuidhinishiwa jumla ya Sh. Bilioni 144.85, ambapo kati ya hizo Sh. Bilioni 126.01 ni kwa matumizi ya kawaida na Sh. Bilioni 18.83 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Katika mwaka huo wa fedha, ofisi imeweka mkazo katika kuimarisha sekta binafsi kama injini ya ukuaji wa uchumi.
Profesa Mkumbo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi, akibainisha kuwa mafanikio ya mageuzi ya uchumi yatategemea uimara, ushindani na ushiriki mpana wa wadau wote.
Amesema juhudi zitaelekezwa katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa (MSMEs), pamoja na vijana, wanawake na makundi maalum ili kushiriki kikamilifu katika uchumi.
Aidha, ofisi itaandaa Taarifa ya Hali ya Sekta Binafsi ili kusaidia maamuzi ya sera na mipango kwa kuzingatia takwimu sahihi.
Sambamba na hilo, amesema Serikali itaboresha mfumo wa majadiliano kati yake na sekta binafsi ili kuhakikisha uwakilishi jumuishi na wenye matokeo chanya kwa maendeleo ya taifa.
Katika juhudi za kupunguza umasikini, ofisi imepanga kuratibu na kufanya tathmini ya programu zote za kupunguza umasikini nchini.
Pia itaandaa Mfumo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji wa Umaskini utakaoweka viashiria, ukusanyaji wa takwimu na matumizi yake katika kupanga sera na bajeti.
Amesisitiza kuwa hatua hizo zinalenga kuhakikisha ukuaji wa uchumi unaenda sambamba na ustawi wa wananchi wote.

You Might Also Like

TEA Kuhakikisha Mazingira Ya Kujifunzia, Kufundishia Yanaboreshwa

Wanufaika wa SDF Waeleza Mafaniko Waliyoyapata

CWT Yatoa Wito Kwa Walimu Kujitokeza Kupiga Kura Oktoba 29 

PBPA Yaagizwa Kuharakisha Upokeaji Na Usambazaji Wa Mafuta Nchini

Profesa Nombo Atembelea Banda la UDSM, 88 Dodoma

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article WASICHANA WAANDIKA HISTORIA MPYA KWENYE MASOMO YA SAYANSI MKOANI SONGWE
Next Article Ufaulu  Wa   Somo La Hisabati  Shida Ya Taifa- Wanu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Sheria Ya  Kuzuia Shisha Kutungwa, Yabainika Kuwekwa Dawa Za Kulevya
Habari May 29, 2026
Waraibu Wa Dawa Za Kulevya 85,425  Wapatiwa Huduma Ya Tiba Nchini Kwa Mwaka 2025
Habari May 29, 2026
NHC Kuendelea Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Kimkakati Ya Ujenzi Wa Nyumba
Habari May 28, 2026
Kutokulipa Kodi Ya Pango La Ardhi Unakosa Sifa Za Kugombea Nafasi Za Uongozi
Habari May 28, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?