MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: WASICHANA WAANDIKA HISTORIA MPYA KWENYE MASOMO YA SAYANSI MKOANI SONGWE
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > WASICHANA WAANDIKA HISTORIA MPYA KWENYE MASOMO YA SAYANSI MKOANI SONGWE
Makala

WASICHANA WAANDIKA HISTORIA MPYA KWENYE MASOMO YA SAYANSI MKOANI SONGWE

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
6 Min Read
Wanafunzi wakifanya mafunzo kwa vitendo ndani ya maabara ya kisasa shule ya Sekondari Ndugu iliyopo Mkoani Songwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.
Hamasa ya maabara na ari ya wanafunzi vyavunja dhana potofu, wasichana waibuka vinara wa masomo ya sayansi.
Na Mwandishi Wetu
Tabasamu la kujiamini linaonekana usoni mwa Sifael Mboma (15), mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Songwe iliyopo wilayani Momba mkoani Songwe.
Licha ya kusoma katika shule iliyoko pembezoni mwa mji, ana ndoto kubwa ya kuwa mhandisi siku moja.
Kwa Sifael, sayansi siyo tu masomo ya darasani bali ni sehemu ya maisha ya kila siku.
Anazungumzia masomo ya sayansi kwa msisimko na kujiamini akieleza namna yanavyomvutia na kumpa mwelekeo wa maisha yake ya baadaye.
“Ukiangalia maisha yetu ya kila siku yamezungukwa na sayansi kama vile uhandisi.
Habari Picha 11776
Wanafunzi Shule ya Sekondari Ndugu iliyopo Wilayani Mbozi, Mkoani Songwe wakiendelea na masomo kwa vitendo katika maabara za sayansi zilizofanyiwa ukarabati kwa ufadhili wa UNICEF ikishirikiana na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
“Tunaishi katika nyumba na majengo yaliyojengwa kwa utaalamu huo,” anasema.
Anapozungumzia masomo ya sayansi, macho yake yanang’aa na uso unakuwa na nuru zaidi ishara ya kumaanisha anachokiamini.
Anaeleza kuwa, majaribio ya vitendo katika maabara hasa kwenye somo la kemia humjengea hamasa ya kujifunza.
Anasema, kuchanganya asidi na besi na kushuhudia matokeo yake papo kwa hapo kwake siyo tu jaribio, ni uzoefu unaochochea bidii kuifikia ndoto yake.
Sifael anasema, sayansi ni daraja la suluhu za changamoto katika jamii.
Habari Picha 11777
Mwalimu wa masomo ya Sayansi Shule ya Sekondari Shiwinga ya Wilayani Mbozi, Songwe Bw. Remmy Mwakifuna akiwa na wanafunzi kwenye  moja ya maabara ya Sayansi iliyofanyiwa ukarabati kwa ufadhili wa UNICEF ikishirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Anaamini kuwa kujikita katika taaluma hizo kutasaidia kuongeza idadi ya wataalamu wa kike katika sekta muhimu kama uhandisi na udaktari.
“Wanawake wanapopata huduma kutoka kwa wataalamu wenzao, wanakuwa huru na kupata faraja zaidi,” anasema.
Sifael pia ana ujumbe mzito kwa wasichana wenzake kuwa waachane na hofu na dhana potofu kwamba masomo ya sayansi ni magumu au ni ya wavulana pekee.
Hadithi ya Sifael si ya kipekee bali ni sehemu ya wimbi jipya la wasichana mkoani Songwe wanaoanza kuonyesha uthubutu katika masomo ya sayansi.
Katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Songwe, mafanikio yanaonekana wazi.
Mkuu wa shule hiyo  Janeth Mwamwile anasema kati ya wanafunzi 25 waliohitimu kidato cha nne mwaka 2025, 12 walipata daraja la kwanza, wanne daraja la pili, wanane daraja la tatu, mmoja daraja la nne na hakuna aliyepata daraja sifuri ishara ya mabadiliko chanya yanayochipuka.
Katika wilaya jirani ya Mbozi, simulizi kama hiyo inaendelea kujitokeza.
Judith Mgode mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Ndugu na Edna Rajab wa kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari Shiwinga, ni miongoni mwa wasichana wanaothibitisha kuwa uwezo wa kufaulu masomo ya sayansi hauchagui jinsia.
Judith anasisitiza kuwa mafanikio yanahitaji bidii na nidhamu, bila kujali somo analosoma mwanafunzi.
Habari Picha 11779
Mwanafunzi Sifael Mbona wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari ya Wasichana Songwe iliyopo Wilayani Momba mkoani Songwe, akiongea mbele ya shule yao jinsi gani wanafurahia miundombinu mizuri na bora iliyofadhiliwa na UNICEF kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) shuleni kwao.
Mabadiliko hayo yanaungwa mkono na takwimu ambapo katika Shule ya Sekondari Ndugu Mkuu wa shule hiyo Cosmas Nzowa anasema, kwa sasa wasichana wanaongoza katika mkondo wa sayansi.
Kati ya wanafunzi 158 wanaosoma masomo ya sayansi, 100 ni wasichana sawa na asilimia 63.2.
Nzowa anahusisha mafanikio hayo na maboresho ya mazingira ya kujifunzia hususan ukarabati wa maabara tatu za sayansi kupitia ushirikiano wa UNICEF na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
“Mwaka jana tulikuwa na wanafunzi 70 wa sayansi, lakini mwaka huu wameongezeka na wamefikia 158 baada ya kukamilika kwa maabara hizi,” anasema.
Katika Shule ya Sekondari Shiwinga, hali ya ujifunzaji wa masomo ya sayansi imebadilika kwa kiasi kikubwa.
Mwalimu wa sayansi Remmy Manfred Mwakifuna anaeleza kuwa awali walikuwa na maabara moja ndogo iliyoweza kuhudumia wanafunzi wachache, hali iliyowalazimu kufanya baadhi ya majaribio darasani.
Kupitia ukarabati huo wa maabara mbili kwenye shule yetu, wanafunzi wanapata fursa ya kujifunza kwa vitendo katika mazingira bora zaidi, anasema  Mwakifuna.
Naye Kaimu Mkuu wa shule hiyo  Ibrahim Nelson Mgalle anasema, anaamini maboresho hayo yataongeza ufaulu wa wanafunzi huku akitoa shukrani kwa Serikali pamoja na wadau wa maendeleo waliofanikisha juhudi hizo za kukamilika kwa maabara za sayansi.
Kwa ujumla, simulizi ya wasichana wa Songwe inaonyesha wazi kuwa mipaka ya kijinsia katika elimu ya sayansi inaanza kuvunjwa.
Ndani ya maabara hizo si kemikali pekee zinazochanganyika ama kufanyiwa majaribio, bali pia ndoto, juhudi na matumaini ya kizazi kipya cha wanawake wataalamu kinatengenezwa na kuandaliwa.

You Might Also Like

Mpulla: Serikali Imetekeleza Hoja Za TUCTA Kuiboresha CMA

MATUKIO YALIYOJIRI KUANZIA JANUARI 2024, HADI SASA DISEMBA 2024:

Madaktari Toka China Waleta Matumaini Barani Afrika

Vijana wa China Waisimulia Afrika Kupitia Video Fupi”

Abubakar Assenga Aomba Ridhaa Ya Wananchi Wa Kilombero Wamchague Tena

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article JOWUTA Yataka Vyombo vya Habari Vishirikishwe Zaidi Mei Mosi Njombe
Next Article Ofisi ya Rais Mipango Yaomba Bilioni 144.85 kwa Bajeti 2026/27
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Makampuni 100 kushiriki maonesho ya OSHA Njombe
Habari April 17, 2026
Ufaulu  Wa   Somo La Hisabati  Shida Ya Taifa- Wanu
Habari April 16, 2026
Ofisi ya Rais Mipango Yaomba Bilioni 144.85 kwa Bajeti 2026/27
Habari April 16, 2026
JOWUTA Yataka Vyombo vya Habari Vishirikishwe Zaidi Mei Mosi Njombe
Habari April 16, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?