MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu, Aongoza Harambee Mei Mosi 2026
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu, Aongoza Harambee Mei Mosi 2026
Habari

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu, Aongoza Harambee Mei Mosi 2026

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
4 Min Read
Zaidi ya Bilioni 1.6 Zaahidiwa
Na Lucy Ngowi
DODOMA: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwinjulu Nchemba, ameongoza hafla ya uchangishaji fedha kwa ajili ya maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka 2026, yatakayofanyika kitaifa mkoani Njombe, huku wadau mbalimbali wakiahidi kuchangia zaidi ya Shilingi bilioni 1.6.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Nchemba amesema Maadhimisho ya Mei Mosi ni jukwaa muhimu la kutambua mchango wa wafanyakazi katika maendeleo endelevu ya taifa, akibainisha kuwa mafanikio ya sekta mbalimbali yanatokana na juhudi zao.
“Tunatambua kazi kubwa inayofanywa na wafanyakazi wa sekta za umma na binafsi. Mei Mosi si tukio la kawaida la kalenda, bali ni siku ya kuenzi mafanikio yanayotokana na juhudi zao kupitia Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA),” amesema.
Habari Picha 11738
Ameongeza kuwa mafanikio hayo yanachangiwa na uwajibikaji wa wafanyakazi katika sekta zote, huku akisisitiza umuhimu wa wadau kuendelea kuunga mkono maandalizi ya sherehe hizo.
Dkt. Nchemba amempongeza Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano ya Viwanda, Deus Sangu, kwa kusimamia vizuri maandalizi hayo na kuweka msukumo katika kufanikisha shughuli hiyo.
Amesema fedha zitakazopatikana zitatumika kugharamia maandalizi ya maadhimisho hayo, na kuwataka wadau kuendelea kujitokeza kwa wingi kuunga mkono jitihada hizo.
Miongoni mwa taasisi zilizotoa ahadi za michango ni Benki ya CRDB (Sh. milioni 100), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Sh. milioni 10, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Sh. milioni 10, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Sh. milioni 30, Benki ya NMB Sh. milioni 80 na Benki ya Azania Sh. milioni 20.
Habari Picha 11739
Wengine ni Bodi ya Mkonge Tanzania (Sh. milioni 20), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Sh. milioni 10, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Sh. milioni 20, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Sh. milioni 35, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Sh. milioni 30 na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Sh. milioni 50.
Pia, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Sh. milioni 20, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Sh. milioni 100, Benki ya Ushirika Tanzania (TCB) Sh. milioni 10, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Sh. milioni 10 na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Sh. milioni 100 walijumuika katika michango hiyo.
Habari Picha 11740
Taasisi nyingine ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Sh. milioni 100, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Ushirika Sh. milioni 20, Wakala wa Serikali Mtandao (e-GA) Sh. milioni 30, taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kazi, Ajira na Mahusiano Sh. milioni 150 pamoja na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Sh. milioni 150.
Habari Picha 11741
Kwa upande wake, Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano  Sangu, amesema uwepo wa Waziri Mkuu katika hafla hiyo ni ishara ya dhamira ya Serikali katika kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na taifa kwa ujumla.
Amesema maandalizi ya Maadhimisho ya Mei Mosi yanaendelea vizuri, ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya uwanja utakaotumika, huku wakitarajia kushirikisha zaidi ya watu 5,000.
Amebainisha kuwa bajeti ya maandalizi hayo ni takribani Sh. Bilioni 5.
Habari Picha 11736
Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya, amesema vyama vya wafanyakazi vitaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyika kwa mafanikio makubwa, akisisitiza ushirikiano huo utaongeza tija kwa wafanyakazi na taifa kwa ujumla.
Habari Picha 11742

You Might Also Like

PBPA Yaagizwa Kuharakisha Upokeaji Na Usambazaji Wa Mafuta Nchini

Tanzania Kuweka Muongozo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Takwimu Kidijitali

TARI Yanufaisha Wadau Wa Kilimo, Ugunduzi Wa Mbegu Bora Na Za Kisas

Vikao vya Kamati za Bunge Kuanza Januari 13, 2026 Dodoma

Ajali Yakatisha Maisha Ya Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji TANESCO, Dereva Wake 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ubunifu Wa Majengo Watakiwa Kuzingatia Tija Na Gharama Nafuu
Next Article Bunge Marathon kufanyika April 18,yakidhi viwango vya kimataifa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Bunge Marathon kufanyika April 18,yakidhi viwango vya kimataifa
Habari April 14, 2026
Ubunifu Wa Majengo Watakiwa Kuzingatia Tija Na Gharama Nafuu
Habari April 11, 2026
Waziri Ulega aridhishwa na miradi ya dharura TANROADS
Habari April 11, 2026
Mbunge Majule ataka wanawake wapewe elimu ya fedha na mitaji
Habari April 11, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?