Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 23

Spika Zungu Atangaza Kifo Cha Mbunge Wa Peramiho, Jenista Mhagama

Na Lucy Ngowi
SPIKA wa Bunge,  Mussa Azzan Zungu, ametangaza kifo cha Mbunge wa Jimbo la Peramiho,  Jenista Mhagama, kilichotokea leo Desemba 11, 2025, Jijini Dodoma.
“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho, Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama, kilichotokea leo tarehe 11 Desemba 2025, Jijini Dodoma,” amesema.
Ametoa pole kwa Wabunge wote, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Peramiho, akiwataka kuwa na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.
Amesema kuwa Ofisi ya Bunge, kwa kushirikiana na familia ya marehemu, inaendelea kuratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitatolewa kadri zitakapopatikana.
Marehemu Jenista  Mhagama alizaliwa Juni 23, 1967 na amefariki dunia leo Desemba 11, 2025.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.