Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 7, 2026
Habari Lucy Ngowi 4

Utiaji Saini Mkataba Wa Ujenzi Jengo La TUGHE Wafanyika

Na Mwandishi Wetu
DODOMA: CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), kimetia saini ya Mkataba wa ujenzi wa jengo lake la Kitega Uchumi, sambamba na kumkabidhi mkandarasi eneo la ujenzi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni jijini Dodoma.
Hafla hio fupi imehudhuriwa na Wajumbe wote wa Baraza Kuu la TUGHE wakiongozwa na Mwenyekiti wa TUGHE Taifa, Joel Kaminyoge aliyeambatana na Viongozi wengine wa Kitaifa wa Chama, Watendaji, Viongozi Wastaafu, Wataalamu wa Ujenzi pamoja na Mkandarasi aliyepewa kazi ya Ujenzi wa Jengo hilo.
Jengo hilo  litakuwa na Ofisi za Makao Makuu ya Chama pamoja sehemu ya Hoteli ya kisasa ambapo itakapokamilika itakuwa ni sehemu ya Kitega Uchumi kitakachoongeza mapato ya Chama.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.