Na Mwandishi Wetu
SPIKA wa Bunge la Tanzania, Mussa Zungu, pamoja na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Yacoub Mohamed, wamefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Saqr Bhogash, katika ofisi za Bunge hilo Abu Dhabi, Novemba 25, 2025.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili, hususan katika upande wa Mabunge.

Aidha, imekubaliwa kuunda kamati ya kudumu ya ushirikiano baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kamati hiyo itaratibu masuala ya pamoja, ikiwemo ziara za Wabunge na Viongozi wa Mabunge ya pande zote mbili kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na mafunzo ya kujengeana uwezo katika masuala ya kibunge.


