MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wizara Yapanga Kunufaika Na Maarifa Ya Mabalozi Wastaafu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wizara Yapanga Kunufaika Na Maarifa Ya Mabalozi Wastaafu
Habari

Wizara Yapanga Kunufaika Na Maarifa Ya Mabalozi Wastaafu

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeanza kuweka utaratibu wa kuvuna maarifa na uzoefu wa Mabalozi Wastaafu ili kuimarisha diplomasia na maendeleo ya taifa katika sekta mbalimbali.
Hatua hiyo imeelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, wakati akifungua kikao cha mashauriano kati ya uongozi wa wizara na Mabalozi Wastaafu kilichofanyika jijini Dar es Salaam Aprili 15, 2026.
Habari Picha 11766
Amesema wizara imeanzisha vikao vya mara kwa mara na Mabalozi hao kwa lengo la kutumia uzoefu wao katika kukuza uhusiano wa kimataifa utakaonufaisha nchi kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Balozi Kombo ametaja baadhi ya maeneo yanayohitaji mchango wao kuwa ni pamoja na kuimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi nyingine, hususan barani Afrika, pamoja na kusaidia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kukuza uchumi kwa kasi na ufanisi.
Habari Picha 11765
Ameongeza kuwa mabadiliko ya dunia, hasa katika teknolojia ya kidigitali, yanahitaji mikakati madhubuti ili taifa linufaike na kukabiliana na changamoto zake.
Pia amesisitiza umuhimu wa uzoefu wao katika kuchambua siasa za kimataifa ambazo zimekuwa na mwelekeo usiotabirika, hali inayoweza kuathiri nchi zinazoendelea.
Aidha, amesema maarifa ya Mabalozi Wastaafu ni muhimu katika kuendeleza taswira chanya ya Tanzania kimataifa, hususan wakati nchi inapopewa majukumu ya uongozi wa kikanda na kimataifa.
Habari Picha 11768
Amebainisha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mwaka 2028, hivyo maandalizi bora yanahitajika.
Awali, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, amesema serikali inaangalia uwezekano wa kuweka mfumo rasmi wa ushirikishwaji wa Mabalozi Wastaafu kupitia Ofisi ya Rais – UTUMISHI ili mchango wao utambulike kisheria.

You Might Also Like

Diwani Kata Ya Majengo Awasihi Wananchi Kufanya Kazi Kwa Bidii

DIT Andaeni Taarifa  Itakayowezesha Wanafunzi Kupelekwa Nje Kujifunza-Mkenda

Chalamila afanya ukaguzi mwenendo wa utoaji huduma Kivuko cha Feri

Msisubiri Kupewa Amri, Ufanyaji Usafi Kwenye Maeneo Yenu – Lugendo

Wagonjwa wa Magonjwa Yasiyoambukiza waongezeka Temeke

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tume Ya Madini Kufuta  Leseni 40 Za Utafutaji Madini 
Next Article JOWUTA Yataka Vyombo vya Habari Vishirikishwe Zaidi Mei Mosi Njombe
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Yaingia Makubaliano Ya Ushirikiano Na DIT Kuimarisha Usimamizi Wa Mataifa
Habari June 8, 2026
Wananchi Waelimishwa Masharti ya Kubadilisha Noti Zilizochakaa, Kuungua na Kuchanika
Habari June 7, 2026
DMI Yawaalika Vijana Kujiunga Na Masomo Ya Ubaharia
Habari June 6, 2026
Taifa Gas Yaendelea Kuongoza Kampeni ya Nishati Safi kwa Taasisi na Sekta ya Utalii Tanzania
Habari June 6, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?