Na Lucy Lyatuu
SHIRIKA la Maendeleo la Wafanyakazi (WDC) lina mpango mkubwa wa maboresho ya miradi yake ya majengo nchini lengo likiwa ni kuongeza kipato na kuongeza Fursa za biashara.
Meneja Mkuu wa WDC, Muchunguzi Kabonaki amesema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na gazeti la MFANYAKAZI kuelezea miradi inayosimamiwa na Shirika hilo na mipango waliyonayo kwa ajili ya mabotesho.
Amesema WDC inajivunia kumiliki majengo mbalimbali nchini ikiwa ni uwekezaji wa wanachama kupata fedha badala ya malimbikizo ya michango.

Ameitaja mikoa ambayo Shirika limeweka vitega uchumi vyake ambavyo ni majengo kuwa ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Moshi.
“Ikumbukwe kuwa WDC ni mwendeshaji wa baadhi ya vitega uchumi vya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi na Kwa Sasa linaendesha vitega uchumi vya makazi,” amesema.