Na Lucy Lyatuu
WIZARA ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema jumla ya walimu 300 wa shule za msingi na sekondari wanapafiwa mafunzo ya TEHAMA yatayayoboresha elimu nchini.
Mafunzo hayo yanafadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF) na yataendeshwa na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu Cha Dodoma na Chuo Kikuu Cha Mbeya (MUST).
Waziri wa Wizara hiyo, Jerry Slaa amesema hayo katika Chuo Cha DIT wakati akifungua mafunzo hayo Kwa walimu 100 ambapo Kila Chuo kitapokea jumla ya walimu 100.
Akizungumza Slaa amesema mafunzo hayo yataziba pengo la kidigitali Kwa kuwashirikisha walimu kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo shule za vijijini.
Amesema hizo zitanufaika kupitia mradi huo wa kuiunganisha shule ulioko chini ya UCSAF Kwa kufikishwa pia vifaa vya Tehama na kuiunganisha mtandao wa intanenti .
Slaa amesema mpaka Sasa shule 210 zimepatiwa vifaa vya Tehama ikiwemo kompyuta,projekta mashine za kuandika na kwamba mafunzo hayo yatawezesha walimu kuvitumia vifaa hivyo Kwa ufanisi.
Amesema chini ya mafunzo hayo pia watajengewa uwezo wa kufanya marekebisho madogo na programu mbalimbali za kidigitali.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya DIT, Profesa Ezekiel Amir amesema mafunzo yatasadia kuboresha mazingira ya ufundishaji, uelimishaji na kurahisisha ufundishaji kupitia vishkwambi na kutoa mitihani.
Amesema ni matumaini yake kuwa watatumia fursa hiyo adimu na wareheapo kwenye vituo vya kazi wawe msaada na kupanua wigo wa TEHAMA katika ufundishaji.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF Peter Mwasalyanda amesema asilimia 98 ya Watanzania wamefikiwa na huduma ya mawasiliani na kwamba Kwa mwaka huu wanatarajia kuwajengea walimu uwezo.