MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TPHPA Yapeleka Wadudu 4,252 Ziwa Victoria Kudhibiti Gugu la Kariba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TPHPA Yapeleka Wadudu 4,252 Ziwa Victoria Kudhibiti Gugu la Kariba
Habari

TPHPA Yapeleka Wadudu 4,252 Ziwa Victoria Kudhibiti Gugu la Kariba

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imechukua hatua ya kudhibiti gugumaji vamizi la Kariba kwa kupeleka wadudu 4,252 katika Ziwa Victoria.
Aidha mayai ya wadudu hao yamepandikizwa kwenye ekari 15 za ziwa hilo, hatua inayolenga kudhibiti ueneaji wa mmea huo hatari.
Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mafanikio ya mamlaka kwa mwaka 2023/2024 hadi 2025/2026, Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Ndunguru, amesema wadudu waliovunwa ni Mbawakavu wakubwa 3,231 na Viluwe luwe zaidi ya 1,021, kisha kusambazwa katika maeneo mbalimbali kuzunguka Ziwa Victoria.
Habari Picha 11584
Profesa Ndunguru amesema gugu la Kariba, lenye jina la kisayansi Salvinia molesta, ni mmea wa kigeni kutoka Brazil, na ripoti ya kwanza ya kuibuka kwa mmea huo Tanzania iliripotiwa Agosti 2024 katika Kivuko cha Busisi, Ziwa Victoria.
Wadudu waliosambazwa husaidia kudhibiti mmea huu vamizi katika maeneo ikiwemo Bwawa la Zungu, Wilaya ya Sengerema, Kijiji cha Rubungo na Bwawa la Nyitundu, Kata ya Kahumulo, Wilaya ya Misungwi.
Athari za gugu la Kariba: Gugu hili linaweza kuathiri vibaya wavuvi na wakulima wa maeneo yanayozunguka ziwa hilo kwa kuziba bwawa, kupunguza uingizaji wa mwanga na oksijeni ndani ya maji, na hivyo kuathiri uhai wa samaki na viumbe wengine wa majini.
 Utafiti wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) unaeleza jinsi matope ya Salvinia yalivyoweza kupunguza oksijeni, kuongeza dioksidi ya kaboni, na kuathiri uzalishaji wa samaki na viumbe wengine wa maji.

You Might Also Like

Kasulu Yaandaa Bonanza La Michezo Kuhamasisha Uchaguzi Mkuu, Mapokezi Ya Mwenge

Taasisi Za Dini Zinazofanya Biashara Zinatakiwa Kulipa Kodi

Mwalim: Ardhi Yetu ni Ufunguo wa Uhuru wa Kiuchumi

Tari Ilonga yaboresha mbegu, mavuno yapanda hadi tani 3.8 kwa hekta

Bodi Ya Usajili Wabunifu Majengo Yapeleka Mahakamani Mashauri 300 Ya Ujenzi Usiozingatia Taratibu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wizara ya Maji Yasisitiza Ushirikiano Na Sekta Binafsi Kuhifadhi Rasilimali za Maji
Next Article UNFPA,Wadau Washauri Kuimarisha Usalama Wa Kidigitali Kukabiliana na Ukatili Wa Jinsia Mtandaoni
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TTCL  Yatumia Tamasha La Kizimkazi Kueleza  Wananchi Fursa Wanazotoa
Makala August 15, 2026
Rais Samia Afurahishwa Na Huduma za NSSF
Habari August 13, 2026
  VETA Yashiriki Tamasha La Kizimkazi
Habari August 13, 2026
Vijana Watakiwa Kuanza Utekelezaji Wa Mipango Waliyonayo
Habari August 12, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?