MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TaSUBa Yahimiza Vijana Kuzifikia Fursa Za Mafunzo Ya Sanàa Na Utamaduni
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TaSUBa Yahimiza Vijana Kuzifikia Fursa Za Mafunzo Ya Sanàa Na Utamaduni
Habari

TaSUBa Yahimiza Vijana Kuzifikia Fursa Za Mafunzo Ya Sanàa Na Utamaduni

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Lucy Lyatuu,Morogoro
TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imewahimiza vijana na wadau wa sanaa nchini kutumia fursa za mafunzo inayotoa ili kukuza vipaji, kuongeza ujuzi na kujenga uwezo wa kujiajiri kupitia sekta ya sanaa na utamaduni.
Akizungumza katika Tamasha la Nne La Taifa La  Utamaduni  linaloendelea mkoani Morogoro, Naibu Mkuu wa TaSUBa, Gabriel Kiiza, amesema taasisi hiyo inatoa programu mbalimbali zinazolenga kuwajengea wanafunzi uwezo katika maeneo tofauti ya sanaa, ikiwemo sanaa za maisha na ufundi, uzalishaji wa filamu na uigizaji, pamoja na uzalishaji wa muziki na sauti.
Kiiza amesema programu hizo zinapatikana katika ngazi za mwaka mmoja kwa ajili ya kupata cheti na miaka miwili kwa ngazi ya diploma, huku TaSUBa pia ikitoa mafunzo ya muda mfupi ya mwezi mmoja hadi miwili kwa watu wanaotaka kuongeza ujuzi katika eneo fulani la sanaa.
Amesema mafunzo ya muda mfupi yanamruhusu mtu mwenye kiwango chochote cha elimu kuchagua eneo analotaka kujiongezea ujuzi, akisisitiza kuwa shughuli za sanaa zinaweza kuwa chanzo cha ajira na kipato kwa mtu binafsi bila kuathiri shughuli nyingine anazofanya.
Amesema vipaji vinahitaji kuendelezwa kwa elimu kwamba mwenye   kipaji cha sanaa anapaswa kupata maarifa na ujuzi unaoweza kumsaidia kukifikisha katika kiwango cha kitaalamu na kumwezesha kutumia kipaji hicho kiuchumi.
Ametoa wito kwa vijana na wadau wa sanaa nchini kuchangamkia fursa hizo, akieleza kuwa TaSUBa imekuwa ikizalisha wahitimu wanaofanya kazi katika taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, huku wengine wakipata fursa ya kuendelea na elimu ya juu ndani na nje ya Tanzania.
 Amesema kwa wanaotaka kujiunga na programu za muda mrefu, TaSUBa inaendelea kupokea maombi hadi Septemba 10, 2026.

You Might Also Like

July 10, 2025

Kikosi Kazi Maalumu Cha Kupitia Muongozo Wa Ufasili Wa Sheria Chazinduliwa

Wizara Yapanga Kunufaika Na Maarifa Ya Mabalozi Wastaafu

Siri ya ushindi JKT hii hapa

Huduma ya Mahakama ya Mwanzo yasogezwa Wilaya ya Ubungo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mfuko Wa Utamaduni Watoa Sh Bil 14.7 Kwa Miradi Ya Sanaa
Next Article TFNC Yahimiza Wanaotoa Ushauri Wa Lishe Mitandaoni Kushirikiana Na Taasisi Zenye Mamlaka
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TFNC Yahimiza Wanaotoa Ushauri Wa Lishe Mitandaoni Kushirikiana Na Taasisi Zenye Mamlaka
Habari August 27, 2026
Mfuko Wa Utamaduni Watoa Sh Bil 14.7 Kwa Miradi Ya Sanaa
Habari August 26, 2026
BMT Kutumia Tamasha La Taifa La  Utamaduni Kuelimisha Wananchi Kuhusu Fursa Za Afcon
Habari August 26, 2026
Teknolojia Ya SmartShamba Planter Yageuza Dakika 30 Kuwa Tumaini La Mkulima
Makala August 25, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?