Na Lucy Lyatuu,Dodoma
JUMUIYA ya Maridhiano Na Amani Tanzania (JMAT) imesema Tanzania hakuna tatizo lolote la kidini wala kiimani na kwamba hakuna kundi lolote li nalonyimwa uhuru,kughasiwa au kuumizwa kwa sababu za kidini.
Katibu wa Jumuiya hiyo, Askofu Ìsrael Maasa .amesema hayo jijini Dodoma kufuatia taarifa iliyotolewa na baadhi ya wabunge wa Kamati ya Mambo ya njenya Bunge la Marekani kuhusu kupitia upya mahusiano kati yaMarekani na Tanzania pamoja namshutuma za ubaguzi wa kidini .

Akizungumza, katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa dini mbalimbali, Katibu amesema Tanzania imejengwa kwa misingi ya umoja wa kitaifa na mshikamano wa kija ii,kuheshimiana kidini na kuishi pamoja kwa amani kwa miongo mingi tangu nchi irate uhuru.
Amesema watanzania bila kujali dinimzao wameishi pamoja kwa amani,kushirikiana katika maendeleo ya taifa,kuoana baina ya fa ilia za dini tofauti,kufanya biashara pamoja,kujenga urafiki na kuendeleza uta aduni wa kuheshi iana ambao u eifa ya Tanzania kuwa miongoni mwa mataifa yenye utuli u mkubwa barani Afrika.
“Shutuma dhidi ya uwepo wa ubaguzi wa kidini nchini Tanzania zinatusikitisha,kutukasirisha na kutufedhehesha, raia wa Marekani wanaoishi Tanzania ni mashahidi wa kusha iri kwa uhuru wa kuabudu nchini,” amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Shekihe Alhad Mussa Salum ameiomba serikali kufanya mapitio ya uhusiano wa kidiplo Asia na ya nchi baina ya Tanzania na Marekani ili pa oja na mambo mengine iweke msimamo wa kukataa na kutovumilia uchonga ishi wa kidini unaoweza kuliingiza taifa kwenye matatizo.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha nia ya dhati ya ku hukua hatua dhidi ya mapungufu ya.iyotokea 2025 ikiwa ni pamoja na kuunda tume ya uchunguzi na nyingine ya kijinai ili uwzjibikaji wz haki na maridhiano vichukue nafasi na kuwezesha kupatikana kwa Katiba mpya kama ambavyo Rais Samia amekwishakuahidi.
Ametoa wito kwa wadau wote wa ndani na njemya nchi kuendelea kuunga mkono mazungumzo ya kujenga ,kuheshimu misingi ya kidiplomasia na kuendeleza ushirikiano unaojenga mahusiano bora baina ya mataifa mbalimbali.

