MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kutokulipa Kodi Ya Pango La Ardhi Unakosa Sifa Za Kugombea Nafasi Za Uongozi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kutokulipa Kodi Ya Pango La Ardhi Unakosa Sifa Za Kugombea Nafasi Za Uongozi
Habari

Kutokulipa Kodi Ya Pango La Ardhi Unakosa Sifa Za Kugombea Nafasi Za Uongozi

Author
By Author
Share
4 Min Read
 Na Lucy Lyatuu,Dodoma

WIZARA Ya Ardhi, Nyumba Na Maendeleo Ya Makazi imesema  kutokulipa kodi ya pango la ardhi ni kosa ambalo linaweza kusababisha kukosa sifa ya kukopesheka katika taasisi za fedha, na vile vile kukosa sifa za kugombea nafasi za Uongozi ikiwemo Udiwani na Ubunge.
Aidha katika mwaka 2026/27, Wizara imepanga kukusanya sh  bilioni 300 kutokana na kodi ya pango la ardhi, ada na tozo mbalimbali zinazohusiana na sekta ya ardhi.
Waziri wa wizara hiyo, Dkt  leonard Akwilapo amesema hayo wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo Bungeni  na kuiomba kuidhinishiwa sh bilioni  210.2  kwa mwaka 2026/27  kwa ajili ya  utekelezaji vipaumbele vya Wizara.
Ametoa rai kwa wamiliki wote wa ardhi kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa msingi wa kulipa kodi ya pango la ardhi, kwa wakati, ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kufutiwa umiliki.
Habari Picha 12247
Kuhusu kukusanya kodi lengo hilo litafikiwa kwa kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo kuendelea kusambaza miundombinu na mifumo ya TEHAMA katika Ofisi za Ardhi za Mikoa na  Halmashauri ili kurahisisha utoaji wa huduma za ardhi.
Amesema pia kuendelea kushirikiana na TAMISEMI kufuatilia halmashauri ambazo hazijakamilisha utekelezaji wa miradi ya KKK; na kuchukua hatua za kisheria kwa wadaiwa sugu ikiwemo kuwafikisha mahakamani.
Aidha, amesema Wizara kwa kushirikiana na mamlaka nyingine inaendelea kutafuta njia bora ya ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi kupitia huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hizo.
Kuhusu hati na nyaraka za Kisheria amesema , katika mwaka 2025/26, Wizara ilipanga kuandaa na kusajili Hatimiliki 500,000, Hati za Hakimiliki ya Kimila 520,000, Hati za Sehemu ya Jengo 1,000, Vyeti vya Ardhi ya Kijiji 100 na Miamala ya Hatimiliki na Nyaraka za Kisheria 100,000.
Amesema hadi Mei 15, 2026 Wizara imeandaa na kusajili Hatimiliki 107,683 sawa na asilimia 21.54 ya lengo; Hati za Hakimiliki ya Kimila 99,762 sawa na asilimia 19.19 ya lengo; Vyeti vya Ardhi ya Kijiji 148 sawa na asilimia 148 ya lengo; na Hati za Sehemu ya Jengo 914 sawa na asilimia 91.4 ya lengo.
Aidha,amesema  jumla ya Miamala ya Hatimiliki na Nyaraka za Kisheria 137,681 zimesajiliwa sawa na asilimia 137.68 ya lengo.
 Katika mwaka 2026/27, Wizara imepanga kuandaa na kusajili Hatimiliki 200,000, Hati za Hakimiliki ya Kimila 300,000, Vyeti vya Ardhi ya Kijiji 60, Hati za Sehemu ya Jengo 1,000 na Miamala ya Hatimiliki na Nyaraka za Kisheria 100,000.
Ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanamiliki ardhi zao kisheria ili kuepuka migogoro na kuwawezesha kutumia ardhi kwa ajili ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Amesema  katika mwaka 2025/26, Wizara ilipanga kutatua migogoro ya ardhi 3,000. Ambapo hadi Mei 15,2026  jumla ya migogoro ya ardhi 5,573 imetatuliwa ambapo kati ya hiyo, migogoro 3,183 imetatuliwa kupitia kliniki za ardhi na migogoro 2,390 imetatuliwa kupitia utaratibu wa kawaida wa kiutawala.
Amesema  katika mwaka 2026/27, Wizara imepanga kushughulikia migogoro 4,000 kiutawala na kutoa rai kwa viongozi, watumishi na wananchi kwa ujumla kuzingatia sheria za ardhi, kanuni na miongozo ili kuepuka kuanzisha migogoro mipya.

You Might Also Like

Mgombea Urais SAU Aahidi Kuongoza Nchi Kwa Hofu Ya Mungu

Ajira kwa Vijana na Afya kwa Wazee: Ajenda Kuu za Wagombea Jimbo la Dodoma Mjini

Mama Mchumgaji TAG Zinga, Asheherekea Siku Ya Kuzaliwa Na Watoto Yatima, Mazingira Magumu

Fema Mining & Drilling Mfano wa Kuigwa – Musukuma

Makalla Aeleza Jinsi CCM Ilivyosimamisha Nchi Mchakato Kura Za Maoni

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tanzania Hakuna Tatizo La Kidini Wala Kiimani-JMAT
Next Article NHC Kuendelea Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Kimkakati Ya Ujenzi Wa Nyumba
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NHC Kuendelea Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Kimkakati Ya Ujenzi Wa Nyumba
Habari May 28, 2026
Tanzania Hakuna Tatizo La Kidini Wala Kiimani-JMAT
Habari May 26, 2026
TUCTA Yawataka Wanahabari Kueneza Elimu ya Fidia kwa Wafanyakazi
Habari May 26, 2026
JOWUTA Yataka Wanahabari Wasajiliwe WCF
Habari May 26, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?