MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania Yaendelea Kuimarisha Usalama Na Ulinzi Wa Taarifa Binafsi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania Yaendelea Kuimarisha Usalama Na Ulinzi Wa Taarifa Binafsi
Habari

Tanzania Yaendelea Kuimarisha Usalama Na Ulinzi Wa Taarifa Binafsi

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na Lucy Lyatuu
TANZANIA  imeendelea kuchukua hatua muhimu katika kuimarisha usalama na ulinzi wa taarifa binafsi katika enzi ya ukuaji wa kasi wa teknolojia za kidijitali, huku Serikali ikisisitiza kuwa ulinzi wa faragha ya wananchi ni msingi muhimu wa kujenga uchumi imara wa kidijitali unaoaminika na jumuishi kuelekea Dira ya Maendeleo 2050.
Kongamano la kwanza la Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi limefunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam likiwa na kaulimbiu isemayo “Faragha ya data kama nguzo kuu: Kulinda mustakabali wa kidijitali jumuishi kuelekea Dira ya 2050, likilenga kuwaleta pamoja wadau kujadili mustakabali wa ulinzi wa taarifa binafsi nchini.
Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Switbert  Mkama, amesema taarifa binafsi ni nyenzo muhimu inayomtambulisha mtu, hivyo ni lazima ilindwe kikamilifu ili kulinda utu, haki na usalama wa wananchi katika mazingira ya kidijitali.
Amesema kwa kuzingatia kasi ya mabadiliko ya teknolojia, hususan ukuaji wa huduma za mtandaoni na mifumo ya kidijitali, Serikali iliona umuhimu wa kuanzisha Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi mwaka 2022 ili kuweka mfumo madhubuti wa usimamizi, elimu na utekelezaji wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi nchini.
Ameongeza kuwa uchumi wa kidijitali hauwezi kujengwa kwa teknolojia pekee, bali unahitaji kiwango kikubwa cha uaminifu na usalama wa taarifa zinazochakatwa na mifumo mbalimbali ya kidijitali, akisisitiza kuwa huduma za serikali na sekta binafsi zinapohamia kidijitali, ulinzi wa taarifa za wananchi ni jambo lisiloepukika.
Habari Picha 12675
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Emmanuel  Mkwilia, amesema kongamano hilo ni la kihistoria kwani ni la kwanza kufanyika tangu kupitishwa kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi mwaka 2022, likitoa fursa ya kutathmini mafanikio yaliyopatikana na kupanga mikakati ya baadaye.
Amesema Tanzania inashuhudia ongezeko kubwa la matumizi ya teknolojia na huduma za kidijitali, hali inayoongeza kasi ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa, hivyo kuhitaji mifumo thabiti ya ulinzi wa taarifa hizo ili kulinda faragha ya wananchi.
Dkt. Mkwilia amesisitiza kuwa faragha ya taarifa binafsi si kikwazo kwa maendeleo ya uchumi wa kidijitali bali ni msingi muhimu unaojenga imani na usalama, akibainisha kuwa bila ulinzi madhubuti wa taarifa, ukuaji wa uchumi wa kidijitali hauwezi kuwa endelevu.
Habari Picha 12676
Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Tume hiyo, Dkt. Adadi  Rajabu, amesema kufanyika kwa kongamano hilo ni hatua muhimu kwa Tanzania katika kuimarisha misingi ya uaminifu, haki na uwajibikaji, jambo litakalosaidia kuongeza imani ya wananchi, wadau na wawekezaji katika mifumo ya kidijitali.
Amesema mabadiliko ya teknolojia, hususan akili unde  (AI) na huduma za mtandaoni, yamefungua fursa kubwa za ubunifu na uwekezaji, lakini yameleta pia hitaji la kuimarisha zaidi ulinzi wa taarifa binafsi bila kuzuia ubunifu huo.
Dkt. Rajabu amesisitiza kuwa maendeleo ya kidijitali yanapaswa kwenda  pamoja na heshima ya utu wa binadamu na misingi ya usalama wa taarifa, akieleza kuwa Tanzania inalenga kuwa kitovu cha ulinzi wa taarifa binafsi kikanda na kimataifa.
Kongamano hilo la siku mbili limeanza  leo Juni 29 hadi julai 01,2026 majadiliano kutoka kwa wataalamu na wadau mbalimbali wa sekta ya TEHAMA, sheria na sekta binafsi, likilenga kuibua suluhisho na mikakati ya kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi nchini.

You Might Also Like

Ofisi ya Rais Mipango Yaomba Bilioni 144.85 kwa Bajeti 2026/27

Serikali Yatumia Zaidi Ya Bilioni 100 Kupeleka Umeme Simiyu

Rais Samia aipongeza TPHPA, kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi, Watendaji

RC Chalamila Ataka Reli Za Ndani Ya Mkoa Kusafirisha Abiria, Kupunguza Msongamano

Tanzania Na Italy Wasaini Makubaliano Kuongeza Ubora Mafunzo Ya Ukarimu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article WCF Yapigia Debe Ushirikiano na Teknolojia Kuimarisha Hifadhi ya Jamii
Next Article Uwekezaji wa Vijana Watajwa Chachu ya Ukuaji wa Uchumi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Uwekezaji wa Vijana Watajwa Chachu ya Ukuaji wa Uchumi
Habari June 29, 2026
WCF Yapigia Debe Ushirikiano na Teknolojia Kuimarisha Hifadhi ya Jamii
Habari June 28, 2026
Sabasaba 2026 Kuingiza Teknolojia Mpya na Fursa za Uwekezaji
Habari June 27, 2026
Benjamin Mkapa Yaanzisha Mfuko Kuchangia Wagonjwa Wa Upandikizaji Figo,Uloto Wasiokuwa Na Uwezo
Habari June 26, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?