MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Rais Samia: Majaji na Mahakimu Simamieni Haki
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Rais Samia: Majaji na Mahakimu Simamieni Haki
Habari

Rais Samia: Majaji na Mahakimu Simamieni Haki

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage, Dodoma
RAIS Samia Suluhu Hassan, amewataka majaji na mahakimu nchini kulinda haki, amani na utulivu kwa mustakabali wa Taifa.
Rais Samia alitoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (TMJA) uliofanyika jijini Dodoma.
Alisisitiza umuhimu wa watoa haki kusimamia misingi ya haki kwa kuzingatia sheria, maadili na viapo vyao bila hofu wala upendeleo.
Habari Picha 10795
Alisema Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025/2050 imejengwa juu ya misingi ya utawala bora, amani, usalama na utulivu, na kwamba mhimili wa Mahakama una nafasi muhimu katika kulinda misingi hiyo.
Aliongeza kuwa Serikali imeanza kuchukua hatua za kuijenga Mahakama imara, inayoaminika na kuheshimika ndani na nje ya nchi.
Akizungumzia changamoto za watumishi wa Mahakama, Rais Samia aliwataka kuwa wavumilivu, akibainisha kuwa Serikali inaendelea kushughulikia maslahi yao hatua kwa hatua.
Aidha, alisema Watanzania wana matumaini makubwa kwa majaji na mahakimu kuona haki, uwazi na utu vikitendeka kwa vitendo.
Habari Picha 10794
Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Masaju, aliwasilisha mapendekezo ya TMJA ikiwemo kuboreshwa kwa maslahi ya watumishi wa Mahakama na kuhamishiwa kwa mashauri yote ya migogoro ya ardhi katika Mahakama kuanzia ngazi ya mwanzo hadi juu, badala ya mabaraza ya ardhi, ili kuondoa mkanganyiko wa kisheria.
Alisema Mahakama iko tayari kushirikiana na Wizara husika na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuandaa marekebisho ya kisheria yatakayowezesha utekelezaji wa mapendekezo hayo.

You Might Also Like

AUWSA Kutibu Maji Taka Yatumike Kwenye Kilimo

Sekta Ya Madini Yapaisha Pato La Taifa

TPHPA: Toeni taarifa mapema milipuko ya kwelea kwelea, nzige, viwavijeshi vamizi inapotokea

Roman Glorig Ahuisha Mkataba wa Uwakilishi wa Heshima wa Tanzania Nchini Czech

Singida Yapokea Zaidi Ya Milioni  Moja 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article CAG Aipongeza TARURA Kwa Ujenzi Wa Miundombinu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CAG Aipongeza TARURA Kwa Ujenzi Wa Miundombinu
Habari January 9, 2026
Tuna Deni La Kusimamia Miradi Na Kusikiliza Kero za wananchi Ili Kuleta Maendeleo Ya Kweli-Salome
Habari January 9, 2026
Rais Dkt Samia Azindua Majengo Ya Kisasa
Habari January 8, 2026
TEA, UNICEF Watekeleza Miradi ya Elimu Visawani Zanzibar
Habari January 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?