MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Nchimbi Ahimiza Ushirikiano wa Wizara Katika Uhifadhi wa Mazingira
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Nchimbi Ahimiza Ushirikiano wa Wizara Katika Uhifadhi wa Mazingira
Habari

Nchimbi Ahimiza Ushirikiano wa Wizara Katika Uhifadhi wa Mazingira

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MAKAMU wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amezitaka wizara zinazohusika na masuala ya mazingira kuongeza juhudi katika kulinda na kuhifadhi mazingira ili Tanzania iwe mfano bora katika uhifadhi endelevu.
Amesema nchi ina rasilimali za misitu pamoja na wataalamu wenye uwezo wa kutosha kufanikisha malengo ya kulinda mazingira.
Habari Picha 11402
Dkt. Nchimbi ametoa kauli hiyo alipokutana na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Masauni na Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew.
Wengine ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Festo Dugange pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Richard Muyungi.
Kikao hicho kilihusisha pia wataalamu kutoka wizara hizo na kilifanyika jijini Dodoma.
Habari Picha 11403
Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa wizara hizo kushirikiana kwa karibu na kuandaa mpango wa pamoja utakaosaidia kulinda mazingira kwa ufanisi zaidi.
Ameeleza kuwa sekta nyingi zinazohusiana na mazingira hutegemea sana uhifadhi wa misitu na rasilimali asili ili kufanikisha majukumu yake.
Ametolea mfano kuwa Wizara ya Maji haiwezi kufanikisha kazi zake ipasavyo ikiwa vyanzo vya maji vitaharibiwa, huku matumizi ya nishati safi ya kupikia yakisaidia kupunguza ukataji holela wa miti.
Aidha, Dkt. Nchimbi amewataka watendaji kuongeza juhudi katika kutekeleza mpango wa kitaifa wa upandaji miti, unaoendana na juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akihamasisha wananchi kupanda miti mara kwa mara, ikiwemo katika maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.
Pia amewataka viongozi hao kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha miti inayopandwa inalindwa na kutunzwa ili kufikia malengo ya kuhifadhi mazingira.

You Might Also Like

Serikali Inaboresha Miundombinu Ya Umeme Kibiti Kuondoa Changamoto Za Umeme – Kapinga

Serikali yazindua Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii na ‘Hifadhi Scheme’ kwa Waliojiajiri

JOWUTA Yawasilisha Ripoti ya Ukaguzi kwa Msajili

Ubovu wa Kituo cha Daladala Bunju Sokoni Watesa Abiria

Silinde Akabidhi Nyaraka za Kufungua Masoko Mapya Nje ya Nchi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mtaka, Ndunguru Wakubaliana Ujenzi wa Maabara ya Kimkakati Njombe
Next Article TPDC Kufikisha Gesi Nchi Nzima  Ndani Ya Miaka Miwili Na Nusu  Kuanzia Sasa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Watendaji Wakuu Waagizwa Kuifanya Dira 2050 Kuwa Mwongozo Wa Maamuzi Yao
Habari July 24, 2026
Nchi za SADC Zahimizwa Kuimarisha Umoja Kukabili Changamoto
Uncategorized July 17, 2026
Wananchi Washauriwa Kutumia  Wataalam Wa Ujenzi Kuepuka Madhara
Habari July 14, 2026
July 14, 2026
Uncategorized July 14, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?