MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: OUT Yazindua Programu Mpya za Masomo Kukidhi Mahitaji ya Uchumi wa Kisasa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > OUT Yazindua Programu Mpya za Masomo Kukidhi Mahitaji ya Uchumi wa Kisasa
Habari

OUT Yazindua Programu Mpya za Masomo Kukidhi Mahitaji ya Uchumi wa Kisasa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DODOMA: CHUO Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimezindua programu mpya za masomo zinazolenga kuandaa wataalamu wenye ujuzi unaohitajika katika uchumi wa kisasa, huku kikitoa wito kwa Watanzania kutumia fursa za elimu zinazotolewa na chuo hicho ili kuongeza maarifa, kujiendeleza kitaaluma na kujiajiri.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa OUT, Dkt. Adam Namamba, amesema chuo hicho kimeendelea kuboresha programu zake ili ziendane na mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya teknolojia.

Amesema kwa mwaka mpya wa masomo, OUT imeanzisha shahada mbalimbali mpya zikiwemo Sayansi ya Kilimo, Sayansi ya Matumizi na Usimamizi wa Rasilimali Nishati, Usalama wa Mitandao na Uchunguzi wa Kidijitali, Teknolojia za Uchakataji wa Chakula, Usimamizi wa Ukarimu na Matukio, Jiografia na Usimamizi wa Mazingira, Historia na Usimamizi wa Urithi wa Utamaduni, pamoja na Usimamizi wa Safari na Utalii.

Habari Picha 12533

“Programu hizi zimeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na ya baadaye ya uchumi ili wahitimu waweze kujiajiri na kushindana katika soko la ajira,” amesema.

Aidha, amesema chuo kimeanzisha programu maalumu ya Uzamili wa Ualimu wa Elimu ya Msingi, inayowawezesha walimu wenye Stashahada ya Ualimu na uzoefu wa kazi wa angalau miaka miwili kuhitimu ngazi ya uzamili ndani ya miaka mitatu.

Dkt. Namamba amesema OUT ni chuo kikuu cha umma kinachotoa elimu kwa njia huria na masafa, hivyo kuwawezesha wanafunzi kusoma wakiwa popote huku wakiendelea na shughuli zao za kazi, biashara au familia.

Amebainisha kuwa chuo kina vituo 32 nchini na kinahudumia wanafunzi kutoka ndani na nje ya

Habari Picha 12534

Pia amesema dirisha la maombi ya uzamili, stashahada za uzamili na uzamivu liko wazi, huku udahili wa cheti, stashahada na shahada kwa mwaka wa masomo 2026/2027 ukitarajiwa kuanza Julai.

Amewahimiza vijana, wafanyakazi, wafanyabiashara na wakulima kutumia fursa hiyo kujiunga na OUT kwa ajili ya kujenga mustakabali wao kupitia elimu bora na nafuu.

You Might Also Like

Samia Mgeni Rasmi Siku Ya Wanawake Jijini Arusha

BRT Kuimarisha Uhusiano Tanzania, China

MOI Kuendesha Kambi Maalum Ya Uchunguzi,  Ushauri Wa Kitabibu Kwa Wazee

Ushirikiano wa TEA, Halmashauri wapewa msukumo kuimarisha mifuko ya elimu

TEN/MET, LHRC Zataka Iwekwe Marufuku Matumizi Ya Viboko

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article BRELA Yahimiza Urasimishaji Biashara  Kuongeza Fursa Za Ukuaji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

BRELA Yahimiza Urasimishaji Biashara  Kuongeza Fursa Za Ukuaji
Habari June 21, 2026
ILO Yazindua Mwongozo Wa Habari Za Uhamiaji, Jowuta Yatia Neno
Habari June 20, 2026
Serikali Yawahamasisha Vijana Kurasimisha Ujuzi Kupitia Programu ya Mama Samia
Habari June 20, 2026
Msigwa Asisitiza Mabonanza Ya Michezo Na Sio Kukusanyika Kuvuruga Amani
Habari June 20, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?