Na Lucy Lyatuu, Dodoma
CHUO Cha Ustawi wa Jamii kimesema kwenye malezi ya watoto kwa sasa kuna changamoto kubwa, na kuwataka wazazi kujitokeza katika chuo hicho na kufundishwa kuhusu malezi ili mtoto aweze kukabiliana na changamoto na kuwa mzalishaji wa uchumi.
Kimesema matukio ya ukatili yanayotokea kwa sasa mengi yanatokana nanmalezi ikianzia kuanzia hatua ya awali mtoto anavyolelewa na hata makuzi yake.
Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dkt Joyce Nyoni amesema hayo wakati akizungumza katika banda la Chuo hicho lililoko katika wiki ya utumishi wa umma inayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park mkoani Dodoma.
Amesema watoto wa sasa wanalelewa kwa kukumbatiwa na mzazi pekee, hawezi kuonywa na jamii, kama ilivyokuwa awali ambapo mtoto alikuwa akilelewa, kuonywa,kufundishwa hata kuelekezwa na jamii.

” Kwa sasa mtoto anakumbatiwa na mzazi peke yake, ambapo awali mtoto alilelewa na kuonywa na jamii lakini kwa sasa amekuwa akikumbatiwa na mzazi peke yake,” amesema Dkt Nyoni na kuongeza kuwa ni muhimu kama mzazi kujitokeza kupata elimu katika Chuo hicho na kufundishwa kuhusu malezi .
Kuhusu huduma ya kisaikolojia itolewayo kwenye mitandao ameitaka jamii kuhudumiwa na watalaam walio sahihi, kwani maofisa ustawi wa jamii wapo katika ngazi ya ofisi za kata,mtaa na hata wilaya.
“Tutafute huduma sehemu stahiki, mtu akihudumu na akiwa hata utaalam husika anaweza kusababisha madhara zaidi hivyo ni muhimu kuwajua walio sahihi,” amesema na kuongeza iwapo mtu anaweza kupata huduma isiyo anaweza kushindwa kujenga uwezo wa kuangalia na kukabiliana na changamoto.
Kuhussu Chuo hicho amesema wapo kwenye wiki ya utumishi wa umma kueleza program mbalimbali wanazotoa pamojamnamdirisha la udahili kwa kozi mbalimbali zitolewazo katika chuo hicho.
Amesema wanatoa program mbalimbali kuanzia ngazinya cheti na uzamili ikiwemo za maendeleo ya jamii,kozi za saikolojia,program za malezi na makuzi ya mtoto.

