MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mamlaka Za Mitaa Ondoeni Urasimu Katika Kuanzisha Biashara Mpya-Waziri Mkuu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mamlaka Za Mitaa Ondoeni Urasimu Katika Kuanzisha Biashara Mpya-Waziri Mkuu
Habari

Mamlaka Za Mitaa Ondoeni Urasimu Katika Kuanzisha Biashara Mpya-Waziri Mkuu

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Lyatuu,Dodoma

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba
amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinaondoa urasimu katika kuanzisha biashara mpya au viwanda vipya katika maeneo yao.
Amesema kwa kufanya hivyo, kutasaidia kuchochea upatikanaji wa ajira mpya kwa vijana, kukuza kipato kwa wawekezaji na wafanyabiashara pamoja na kukuza pato la Taifa.
Habari Picha 11433
Kadhalika amezitaka mamlaka   hizo kuweka mikakati ya kushughulikia changamoto mbalimbali zikiwemo za tozo zisizo rafiki kwa sekta binafsi.
 Dkt Nchemba amesema hayo katika
 wakati akifunga Mkutano wa Kuhakiki Rasimu ya Pili ya Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (Mkumbi II) uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage, HAZINA, jijini hapa.
Akizungumza amewataka Wakuu wa Mikoa na watendaji wao katika mikoa yote nchini kujipanga kutoa taarifa kuhusu uwekezaji na ukuzaji wa biashara kwenye mikoa yao kila wanapotoa taarifa kwa viongozi wa kitaifa.
Habari Picha 11434
“ Ni muhimu Kwa nafasi zenu Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha mnabeba jukumu la kuwa mabalozi  wa uwekezaji katika maeneo yenu kwa kutambua na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika maeneo mliyopo,” amesema.
Amesema Kila  Kiongozi wa mkoa aahakikishe anapotoa taarifa aeleze ameongeza uwekezaji kwa kiasi gani, amekuza biashara kwa kiwango gani na katika kuongeza biashara mpya
Amesema mapendekezo yote yaliyowasilishwa na washiriki wa mkutano huo ambao ni Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na Wakurugenzi yaandaliwe katika mfumo wa mkakati wa utekelezaji ili kuwezesha utekelezaji wake kwa ufanisi.
Amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alishasema isiwepo sheria inayoleta kikwazo katika utendaji kazi wa serikali. Haya tuliyoyabaini, tuyaweke kwenye majedwali na kubainisha lipi ni kikwazo na lipi limefanyika. Leteni hayo mapendekezo.”
“Kuhusu suala la utitiri wa taasisi za udhibiti na kodi, andaeni mapendekezo mahsusi na yawasilishwe kwa Waziri wa Fedha ili yaweze kuingizwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka huu. Hatua hii inalenga kuwa sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini,” amesema
Habari Picha 11435
Awali  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa  Kitila Mkumbo amewashukuru Wakuu wa Mikoa yote kwa ushirikiano wao na jinsi walivyolipa kipaumbele suala la uwekezaji kwenye maeneo yao.
Amesema ofisi yake kwa kushirikiana na Waziri wa Nchi, OWM – TAMISEMI wanaandaa nyenzo za kushindanisha mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa  katika kuvutia uwekezaji na kulinda biashara.
Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar amewaeleza washiriki wa mkutano huo kwamba matarajio ya Serikali kwenye utekelezaji wa DIRA 2050 unaendana na MKUMBI II kwenye maeneo yao.
Amesema Uchumi wa Tanzania  kwa sasa ni dola za Marekani bilioni 100 ikichanganywa  na uzalishaji wa bidhaa zote, huduma na biashara za ndani na za nje .
” Katika miaka 25 ijayo, tunataka tufikie dola za Marekani trilioni moja, maana yake tukue zaidi ya mara 10.” amesema.

You Might Also Like

Dkt Biteko Ampongeza Mwanafunzi Aliyeelezea Miradi Ya Umeme

Silaa Atembelea Banda La NEMC, Wiki Ya Anwani Za Makazi

CATC yawaita wakulima kusomea urushaji wa ndege nyuki

Salum Mwalim: Nitarejesha Hadhi ya Kanda ya Ziwa na Kuinua Zao la Pamba

Daktari: Saratani ya Matiti Inazuilika, Inatibika

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ofisi Ya Taifa Ya Takwimu  Kufanya Tafiti Kwa Wakala Wa Huduma Za Fedha,Viwandani
Next Article Vita Mashariki ya Kati Vyatikisa Uchumi wa SADC, Mawaziri Watakiwa Kuchukua Hatua
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vita Mashariki ya Kati Vyatikisa Uchumi wa SADC, Mawaziri Watakiwa Kuchukua Hatua
Habari March 12, 2026
Ofisi Ya Taifa Ya Takwimu  Kufanya Tafiti Kwa Wakala Wa Huduma Za Fedha,Viwandani
Habari March 12, 2026
GCLA  Yanunua Mitambo Mikubwa Inayogharimu Sh Bil 32.25 Kuimarisha Uchunguzi Wa Sampuli
Habari March 12, 2026
TPDC Kufikisha Gesi Nchi Nzima  Ndani Ya Miaka Miwili Na Nusu  Kuanzia Sasa
Habari March 11, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?