MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Jafo Ahoji Fedha Za Ujenzi Barabara Ya Mzenga – Kisarawe
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Jafo Ahoji Fedha Za Ujenzi Barabara Ya Mzenga – Kisarawe
Habari

Jafo Ahoji Fedha Za Ujenzi Barabara Ya Mzenga – Kisarawe

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
MBUNGE wa Kisarawe (CCM), Seleman Jafo, amehoji mpango wa Serikali wa kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara ya Mzenga–Kisarawe yenye urefu wa kilometa 70 kwa kiwango cha lami.
Jafo amesema barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi wa Kisarawe kwani itachochea ukuaji wa uchumi kwa wakazi wa Mkoa wa Pwani na maeneo ya jirani.
Aliuliza swali hilo bungeni kwa Wizara ya Ujenzi wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya, alisema Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo.
Kasekenya alisema Serikali imeshatambua umuhimu wa barabara hiyo na itaendelea kuitengea fedha kadri zitakavyopatikana hadi ujenzi wake ukamilike kwa kiwango cha lami.
“Tutaendelea kuongeza fedha kadri zitakavyopatikana ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kutokana na umuhimu wake,” alisema Kasekenya.
Katika swali la msingi, Mbunge wa Kibaha Vijijini (CCM), Hamoud Jumaa, alitaka kujua mpango wa Serikali kuhusu ujenzi wa barabara ya Chalinze–Gwata–Magindu–Mpalu–Utete–Rufiji–Tumbi–Boko–Sofa na Korogwe–Sofa.
Akijibu swali hilo, Kasekenya alisema taratibu za manunuzi zinaendelea ili kumpata mshauri atakayefanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara mpya ya Chalinze hadi Utete yenye urefu wa kilometa 354.9 kupitia Bwawa la Julius Nyerere (NHPP).
Aliongeza kuwa usanifu huo unajumuisha kipande cha barabara ya Chalinze hadi Magindu chenye urefu wa kilometa 22.61.
Baada ya kazi za usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo.

You Might Also Like

Waziri Mkuu Ashiriki Kumuombea Baba Wa Taifa

Rais Samia Aipa Neema Miradi Ya Kuzalisha Umeme Iringa

Zaidi Ya Wanachama 800 Wa TUGHE Watembelea Hifadhi Ya Mlima Kilimanjaro

Mchome: Ubunifu wa VETA Ni Mkubwa, Sasa Ni Wakati Wa Uzalishaji Kwa Wingi

BRT Kuimarisha Uhusiano Tanzania, China

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Hakuna Mabadiliko Ya Vituo Vya Kazi Kwa Watumishi Wapya Wa Umma Kwa Sasa -Kikwete
Next Article Serikali Yachukua Hatua Madhubuti Kukuza Ajira kwa Wahitimu wa Vyuo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

VETA -Dakawa Kufundisha Namna Ya Kutunza  Mifugo Kupandisha Thamani Ya Ngozi
Habari August 28, 2026
“Tumejiandaa Vyema Kuzifikia Fursa Za Afcon Kupitia Utalii”-VETA
Habari August 28, 2026
VETA Yaonesha  Mavazi, Bidhaa Za  Utamaduni Kwa Umahiri Katika Tamasha La Utamaduni
Habari August 28, 2026
TPHPA yawataka wakulima, wafanyabiashara kulinda ubora wa mazao, yafungua soko la viazi Zambia
Habari August 27, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?