MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Hatuwezi Kukwepa Matumizi Ya Bioteknolojia – Dkt.Nguvila
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Hatuwezi Kukwepa Matumizi Ya Bioteknolojia – Dkt.Nguvila
Habari

Hatuwezi Kukwepa Matumizi Ya Bioteknolojia – Dkt.Nguvila

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: TANZANIA haiwezi kukwepa kutumia bioteknolojia katika kuendeleza sekta mbalimbali za uchumi na huduma kwa jamii.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Toba Nguvila alipokuwa akimwakilisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Cyprian Luhemeja, katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST).

Amesema hiyo ni kutokana na ukweli kuwa, nchi zilizowekeza katika bioteknolojia ya kisasa zimeweza kupata faida kubwa katika sekta mbalimbali za uchumi na huduma kwa jamii.

“Utandawazi unaoendelea duniani umefanikisha maendeleo ya teknolojia mbalimbali na ueneaji wake ulimwenguni kote,” amesema.

Amesema pamoja na kwamba Tanzania haiwezi kukwepa baiteknolojia, kuna baadhi ya wadau ambao wana mashaka au wanapinga matumizi ya teknolojia hiyo hususan katika sekta ya kilimo.

“Hali  hii inasababishwa kwa kiasi kikubwa na uelewa mdogo wa dhana ya teknolojia hii hata miongoni mwa wanasiasa, watendaji wa serikali, wataalamu na jamii kwa ujumla,”amesema.

Amesema serikali imeweka mfumo thabiti kuhakikisha kuwa utafiti wa kutumia bioteknolojia ya kisasa unafanyika kwa usalama,

Pia bidhaa zozote zinazotokana na teknolojia zitaruhusiwa kutumika baada ya mamlaka za udhibiti kujiridhisha kuwa bidhaa hizo hazina madhara yeyote kwa afya za binadamu, wanyama na kwa mazingira.

Naye Mwenyekiti wa BST, Profesa Peter Msolla  amesema matumizi ya bioteknolojia duniani yameshika kasi kwa kutambua manufaa makubwa yanayopatikana kwenye kilimo, afya, mifugo, viwanda, mazingira, nishati na mifumo mbalimbali zimechangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

0

“Hapa nchini tumeshuhudia ongezeko la bidhaa zitokanazo na bioteknolojia kama viuatilifu, vyakula, mazao na mifugo bora yenye tija kwa mkulima, mbinu za kubadilisha taka za mashambani na viwandani kuwa mbolea na gesi,

“Viuatilifu vya kibiolojia vya kuua viluwiluwi vya mbu, viuatilifu vya kibiolojia kwa ajili ya kuua wadudu waharibifu wanaoshambulia mimea na mazao shambani, hii ikiwa ni mifano michache tu,”amesema.

 

You Might Also Like

Katibu Mkuu CCM Dkt. Nchimbi Akutana na Katibu Mkuu CRC

Wadau Wakaribishwa Kuwekeza Katika Uchakataji, Biashara ya Mkonge Nchini

Tanzania, Ufini Kushirikiana Teknolojia Za Kisasa Sekta ya Misitu

TSB Yasisitiza Umuhimu Kuwekeza Kwenye Uchakataji Wa Mkonge

Fursa za Uwekezaji Kanda ya Ziwa: Buzwagi na Maeneo Mengine ya Kimkakati

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article ‘Skills For Their Future’ Yanufaisha Wanafunzi Zaidi Ya 1000, Walimu 64 
Next Article Kumekucha Uzinduzi wa Washirika wa Tamasha, Tuzo Za Filamu Tanzania 2025
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Kisasa Design: Kampuni ya Kitanzania Inayobadilisha Sekta ya Interior Design na Utengenezaji wa Samani
Habari June 6, 2026
Vidukari Hatari Vyafuatiliwa Mikoa 17 Kulinda Zao la Mpunga
Makala June 5, 2026
KARIBU ESCAPE LODGE SERENGETI – NYUMBA YAKO YA KIFAHARI KATIKATI YA UFALME WA WANYAMAPORI
Habari June 5, 2026
Sheria Ya  Kuzuia Shisha Kutungwa, Yabainika Kuwekwa Dawa Za Kulevya
Habari May 29, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?