MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Rais Mwinyi Azindua Ripoti ya Jiolojia, Utafiti Madini zanzibar
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Rais Mwinyi Azindua Ripoti ya Jiolojia, Utafiti Madini zanzibar
Habari

Rais Mwinyi Azindua Ripoti ya Jiolojia, Utafiti Madini zanzibar

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na  Mwandishi wetu Zanzibar
ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Hussein Ali Mwinyi amezindua Ripoti ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Zanzibar.
Uzinduzi huo umefanyika kwa ushirikiano kati ya Wataalamu kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar (WMNMZ).
Akizindua ripoti hiyo, Mwinyi amewapongeza  wataalamu hao kwa kazi nzuri iliyofanyika ya kubainisha aina ya madini na mahali yaliyopo visiwani humo.
Amesema ripoti hiyo ya Jiolojia itatumika kwenye sekta mtambuka zikiwemo madini, nishati,maji, ujenzi, kilimo, elimu, afya na utalii ambazo ni muhimu katika ustawi wa jamii na uchumi wa Zanzibar.
Katikq uzinduzi huo, Rais Mwinyi ameitaka Wizara ya Maji, Nishati na Madini ya Zanzibar kuhakikisha inaisambaza ripoti hiyo kwa taasisi zote zinazoguswa na tafiti hizo ili kuifanyia kazi kwa manufaa ya Taifa na kuongeza tija kwenye uchumi wa nchi.
Pia Rais Mwinyi ameitaka Wizara ya Madini kupitia taasisi ya GST kudumisha mashirikiano yaliyopo katika Sekta ya Madini na kusisitiza kuendelea kufanya tafiti mbalimbali kwa lengo la kuendelea kugundua maeneo mapya yenye viashiria vya madini, fursa za  utalii na maeneo yenye majanga ya asili nchini.
Pamoja na mambo mengine, Rais Mwinyi ametoa Vyeti kwa wataalamu walioshiriki kufanya tafiti na kuandaa ripoti hiyo kama pongezi na kumbukumbu kwa wataalamu hao.
Kwa upande wake, Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema utafiti uliyofanyika visiwani Zanzibar utawezesha uimarikaji wa uchumi katika visiwa hivyo na kubadilisha maisha ya watanzania wanaoishi visiwani humo.
Waziri Mavunde amesema matarajio ya matokeo ya utafiti huo yatatumika kuvutia uwekezaji mkubwa na kuchochea uchumi wa Taifa.
Naye, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Shaibu Kaduara amesema utafiti uliofanyika katika visiwa hivyo ni utafiti wa awali utakaohitaji kufanyika kwa utafiti wa kina ili kubaini kiwango cha Madini yaliyopo visiwani humo.
Awali, Mkurugenzi Idara ya Nishati na Madini, Said Mdungi amesema Zanzibar kuna Jiolojia ya miamba tabaka ambapo alitaja aina za hiyo miamba, udongo na viashiria vya miamba yenye maji.
Kwa upande wa madini amesema miongoni mwao ni madini tembo, madini ujenzi, chokaa na silica.

You Might Also Like

CHAUMMA Yataka Kuvunja Bodi ya Korosho, Kuunda Mamlaka Mpya ya Mazao ya Kimkakati

Makalla aitaka Halmashauri Longido kutenga fedha, ujenzi wa uzio Samia Girls

Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana

Serikali Inatoa Kipaumbele Kufikisha Umeme Taasis Zinazotoa Huduma Kwa Jamii- Kapinga

TEA, UNICEF na Canada waendeleza mageuzi ya elimu Sikonge

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Swahili International Tourism Expo Kufanyika Oktoba 11 hadi 13
Next Article TRA Kuzindua Boti Za Kisasa Kudhibiti Bidhaa Hatarishi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tume Ya Ulinzi Wa Taarifa Binafsi Yatoa Siku Saba Kwa Taasisi Kujisajili
Habari June 12, 2026
Teknolojia Ya Juisi YA Ndizi Kali Yafungua Fursa Mpya Za Viwanda, Ajira
Makala Uncategorized June 12, 2026
Serikali Yaingia Makubaliano Ya Ushirikiano Na DIT Kuimarisha Usimamizi Wa Mataifa
Habari June 8, 2026
Wananchi Waelimishwa Masharti ya Kubadilisha Noti Zilizochakaa, Kuungua na Kuchanika
Habari June 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?