MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Bidhaa Zinazozalishwa Nchini Zifikie Viwango Vinavyotakiwa Kukidhi Masoko-Balozi Mussa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Bidhaa Zinazozalishwa Nchini Zifikie Viwango Vinavyotakiwa Kukidhi Masoko-Balozi Mussa
Habari

Bidhaa Zinazozalishwa Nchini Zifikie Viwango Vinavyotakiwa Kukidhi Masoko-Balozi Mussa

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Lucy Lyatuu,Dodoma
WAZIRI wa Fedha, Balozi  Khamis  Mussa Omari, amesisitiza umuhimu wa kuwaunganisha wazalishaji na masoko pamoja na kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinafikia viwango vinavyotakiwa pamoja kuzitangaza  ili zifahamike na kupata masoko.
Aidha amewataka , wadau kuongeza juhudi za kutangaza bidhaa za ndani na kuchagiza kuwa  uzalishaji wenye tija hauwezi kuwa na maana endapo bidhaa hazitafika sokoni kwa ubora, kiasi na wakati unaohitajika.
Khamis amesema hayo katika  ziara yake katika Maonesho ya Nane Nane jijini Dodoma, ambapo ametembelea mabanda mbalimbali

Habari Picha 13035

Habari Picha 13033

yanayohusisha wadau wa kilimo, mifugo, uvuvi na sekta zinazohusiana na uzalishaji, akisisitiza umuhimu wa Serikali kuweka nguvu pamoja kuanzia uzalishaji, usindikaji, upatikanaji wa mitaji hadi masoko.

Akiwa katika maonesho haho, amezitaka wizara na taasisi za Serikali kuacha kufanya kazi kwa mtazamo wa kila sekta kivyake na badala yake kuunganisha nguvu katika kuongeza uzalishaji wa kilimo, mifugo na uvuvi, akisema ushirikiano huo ni muhimu katika kuongeza tija na kukuza uchumi wa Taifa.
Amesema wizara zinazohusika na fedha, kilimo, mifugo, uvuvi na viwanda zinapaswa kufanya kazi kwa mtazamo mmoja ili kutatua changamoto zinazowakabili wazalishaji, huku akisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika utafiti utakaosaidia kubaini vikwazo vya uzalishaji na kupata suluhisho zenye uwezo wa kuongeza tija.
Habari Picha 13036
“Mbali ya kusema niko  kwenye kilimo,  niko kwenye fedha, mimi niko viwanda, tunahitaji kwenye maendeleo ya uzalishaji katika sekta ya kilimo, pamoja na mchakato wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, pamoja na huduma ambazo zinaambatana na hili,” amesema Khamis.
Habari Picha 13034
Kuhusu sekta ya uvuvi, Waziri huyo amesema Serikali inapaswa kuendelea kuunga mkono ufugaji wa samaki kutokana na umuhimu wake katika kuongeza upatikanaji wa chakula chenye protini, akibainisha kuwa changamoto zinazoikabili sekta ya uvuvi wa asili katika bahari na maziwa zinaifanya Tanzania kuhitaji kuongeza uzalishaji kupitia njia mbadala.

You Might Also Like

Kuhusisha Wanafunzi Matukio Ya Kisayansi, Kunawafanya Waipende 

Maabara Za Sayansi Zachochea Hamasa Kitaaluma

Timu Wizara Ya Nishati Zawasili Tayari Kwa Bonanza

Nyavu za Plastiki Zatishia Afya za Watumiaji wa Samaki Ziwa Victoria

Mgombea Udiwani Manyoni Adhalilishwa, Rushwa Yadaiwa Kuvuruga Kura Za Maoni

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article  DIB Kulinda Fedha Za Wawekaji Amana Katika Taasisi Za Fedha
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

 DIB Kulinda Fedha Za Wawekaji Amana Katika Taasisi Za Fedha
Habari August 2, 2026
TAFIRI Yaleta Mageuzi Makubwa Ya Uvuvi Kupitia Teknolojia Ya Satelite
Habari August 2, 2026
TADB Yapongezwa Kwa Kuuongeza Uzalishaji Wa Mazao Nchini,Kuinua Kipato
Habari August 2, 2026
SmartDarasa: Tunda la Miaka 40 ya COSTECH Linalobadili Elimu ya Sayansi Tanzania
Makala August 1, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?