MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TAFIRI Yaleta Mageuzi Makubwa Ya Uvuvi Kupitia Teknolojia Ya Satelite
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TAFIRI Yaleta Mageuzi Makubwa Ya Uvuvi Kupitia Teknolojia Ya Satelite
Habari

TAFIRI Yaleta Mageuzi Makubwa Ya Uvuvi Kupitia Teknolojia Ya Satelite

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu,Dodoma
TAASISI Ya Utafiti  Ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) imebainisha kuwa mfumo wa kidigitali unaotumia teknolojia ya satelite wa vua,uza na nunua  (PFZ) unasaidia  wavuvi kutambua maeneo yenye uwezekano mkubwa wa kuwa na samaki.
Tayari mfumo huo umesajili wavuvi zaidi ya 1000 nchini na unawasaidia wavuvi  kupata maeneo yenye uwezekano mkubwa wa kuwa na samaki, ambapo wananchi zaidi ya 3,000 wamekuwa wakiulizia taarifa za maeneo ya kuvua kupitia mfumo huo
Mkurugenzi Mkuu wa TAFIRI, Dkt. Ismael Kimirei, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma  kwenye maonesho ya kilimo Nanenane.
Habari Picha 13018

Habari Picha 13019

 Dkt. Kimirei, mvuvi anaweza kutuma ujumbe kwa simu akieleza eneo alipo na anapopanga kwenda kuvua, ambapo mfumo hutumia taarifa hizo na kutoa mapendekezo ya maeneo yenye samaki wengi.
“Baada ya kuvua, mvuvi hutuma picha ya samaki alionasa na taarifa hizo kupitia mfumo huo, jambo linalomwezesha mnunuzi kumtafuta moja kwa moja bila kupitia kwa madalali,”amesema.
Dkt. Kimirei amesema mfumo huo pia unasaidia wavuvi kupata fursa ya kukopesheka kutokana na taarifa za shughuli zao za kifedha zinazohifadhiwa ndani ya mfumo.
Amesema TAFIRI pia  imeanza kutumia teknolojia ya kupima ubora wa maji kwenye mabwawa ya ufugaji wa samaki ili kuwasaidia wafugaji kubaini mapema mazingira yanayoweza kuhatarisha uzalishaji.
Habari Picha 13020
“Teknolojia hiyo kwa sasa imeanza kutumika mkoani Mwanza kwa kushirikiana na vikundi vya vijana wa BBT pamoja na baadhi ya wananchi, huku lengo likiwa kuwafikia wafugaji wengi zaidi nchini”,amesema.
Amefafanua  kuwa vifaa hivyo vinaweza kutoa taarifa za mapema kuhusu mabadiliko ya mazingira ya maji, ikiwemo uchafuzi wa maji, upungufu wa oksijeni na kushuka kwa joto la maji, hali zinazoweza kuhatarisha maisha ya samaki.
Dkt Kimerei amesema teknolojia hiyo inamwezesha mfugaji kujua mapema kama mazingira ya maji hayako salama kwa samaki vilevile mfugaji  kuchukua hatua haraka za  kuvuna samaki  au kutafuta suluhisho kabla ya kupata hasara.
Amewataka wavuvi na wadau wa sekta ya uvuvi kutembelea banda la TAFIRI katika maonesho ya Nanenane kupata elimu zaidi na kuendelea kujisajili na kutumia teknolojia hizo ili kupunguza gharama za kwenda kuvua bila uhakika wa kupata mavuno.

You Might Also Like

Bodi Ya Wadhamini Ya NSSF Yaridhishwa Na Uwekezaji Wa Ubia Na Jeshi La Magereza

Serikali imejipanga Mkakati wa Taifa wa Matumìzi ya nishati safi ya kupikia – Mramba

Wazazi washauriwa kusomesha watoto useremala

Profesa Ndunguru Abainisha Mwelekeo Mpya Wa Mageuzi Ya Kilimo Duniani

eGA Yatengeneza  Mifumo  Kurahisisha  Kazi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TADB Yapongezwa Kwa Kuuongeza Uzalishaji Wa Mazao Nchini,Kuinua Kipato
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TADB Yapongezwa Kwa Kuuongeza Uzalishaji Wa Mazao Nchini,Kuinua Kipato
Habari August 2, 2026
SmartDarasa: Tunda la Miaka 40 ya COSTECH Linalobadili Elimu ya Sayansi Tanzania
Makala August 1, 2026
TVLA Yazalisha Chanjo ya Kudhibiti Homa ya Kutupa Mimba kwa Mifugo
Habari August 1, 2026
Halmashauri Ya Jiji La Dodoma Lawataka Wakulima Kutumia Nanenane Kujifunza Kilimo Cha Kisasa
Habari August 1, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?