MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: SmartDarasa: Tunda la Miaka 40 ya COSTECH Linalobadili Elimu ya Sayansi Tanzania
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > SmartDarasa: Tunda la Miaka 40 ya COSTECH Linalobadili Elimu ya Sayansi Tanzania
Makala

SmartDarasa: Tunda la Miaka 40 ya COSTECH Linalobadili Elimu ya Sayansi Tanzania

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
12 Min Read

Mwanzilishi wa SmartDarasa, Mhandisi wa Mawasiliano Elias Elisante (Kushoto) na Mwanzilishi mwenza wa SmartDarasa, Kusiluka Aginiwe

Na Lucy Ngowi
KWA zaidi ya miaka 40, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeendelea kujenga mazingira yanayowezesha sayansi, teknolojia na ubunifu kuwa nguzo ya maendeleo ya Tanzania.
Katika kipindi hicho, uwekezaji katika tafiti, ukuzaji wa wabunifu na uatamiaji wa biashara za teknolojia umebadili mawazo ya Watanzania kuwa suluhisho zinazogusa maisha ya wananchi.
Miongoni mwa mafanikio yanayoakisi safari hiyo ni SmartDarasa, ubunifu wa Kitanzania unaobadilisha namna elimu ya sayansi inavyofundishwa.
Kwa miaka mingi, wanafunzi katika shule nyingi za serikali walikabiliwa na changamoto ya kujifunza sayansi kwa vitendo kutokana na upungufu wa maabara na vifaa vya kufanyia majaribio.
Wengi walijifunza kwa nadharia, wakakariri kanuni na kutegemea maelezo ya walimu badala ya kufanya majaribio yaliyowasaidia kuelewa dhana za kisayansi kwa kina.
Changamoto hiyo ndiyo iliyozaa wazo la SmartDarasa, teknolojia ya elimu (EdTech) inayowezesha walimu na wanafunzi kutumia maabara za kidijitali, video za masomo, tathmini na maudhui shirikishi yanayorahisisha ufundishaji na ujifunzaji hata katika shule zisizo na maabara za kutosha.
Mwanzilishi wa SmartDarasa, Mhandisi wa Mawasiliano Elias Elisante, anasema wazo hilo lilitokana na uzoefu wake akiwa mwanafunzi na kuona pengo lililokuwapo katika ufundishaji wa sayansi.
“Tuliona sayansi inafundishwa kwa nadharia sana na kwa kukariri badala ya kuelewa kwa vitendo. Hilo ndilo lililotupa chachu ya kutengeneza teknolojia ambayo ingewezesha mwanafunzi kujifunza sayansi kwa vitendo popote alipo,” anasema.
Safari ya SmartDarasa ilianza mwaka 2019 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kabla ya kuingia hatua ya kibiashara mwaka 2021.
Anasema kadiri ilivyokua, iliibua kuanzishwa kwa kampuni ya Ekima Interactive kupitia muungano na Smartcore, ikiwa na lengo la kutoa suluhisho za kidijitali katika sekta ya elimu.
Tofauti na mfumo wa kawaida unaotegemea vitabu pekee, Ekima Interactive humwezesha mwanafunzi kuona, kushiriki na kujifunza kwa vitendo huku mwalimu akitumia zana za kisasa zinazoboresha ubora wa ufundishaji.
Hata hivyo, safari hiyo isingefika hatua ilipo bila uwekezaji wa Serikali kupitia COSTECH.
Mafanikio ya SmartDarasa ni ushahidi wa namna sera za Serikali za kuwekeza katika sayansi, teknolojia na ubunifu zilivyoanza kuzaa matunda baada ya miongo minne ya kujenga mazingira rafiki kwa wabunifu wa ndani.
Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kituo cha Dar es Salaam cha Uatamiaji wa Biashara za Teknolojia (DTBi-BUNI), Elia Kinshaga, anasema SmartDarasa ni mfano halisi wa jinsi uwekezaji katika sayansi, teknolojia na ubunifu unavyoweza kubadilisha sekta muhimu kama elimu.
Anasema COSTECH ilitoa zaidi ya Sh. Milioni 60 kuwezesha maendeleo ya ubunifu huo kutoka hatua ya wazo hadi kuwa bidhaa yenye uwezo wa kutumika kwa kiwango kikubwa.
“Uwekezaji huo uliwezesha uendelezaji wa teknolojia, uboreshaji wa bidhaa, majaribio ya mfumo na maandalizi ya kuingia sokoni,” anasema.
Mbali na ufadhili wa kifedha, SmartDarasa ilinufaika na huduma za uatamiaji wa biashara kupitia DTBi, kampuni tanzu ya COSTECH iliyoanzishwa mwaka 2011 kusaidia biashara changa za teknolojia.
Anasema kupitia DTBi, kampuni hiyo ilipata ushauri wa kitaalamu, mafunzo ya biashara, usajili wa haki miliki, maandalizi ya uwekezaji na fursa za kuunganishwa na wadau mbalimbali.
Kwamba, hatua hizo ziliiwezesha SmartDarasa kupata ufadhili wa dola za Marekani 70,000 kutoka Mastercard Foundation, fedha zilizosaidia kupanua matumizi ya mfumo huo.
Hayo ni matokeo ya safari ya miaka 40 ya COSTECH ya kuwekeza katika tafiti, sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuzalisha suluhisho zinazotatua changamoto halisi za jamii.
Anaeleza uwekezaji huo umewezesha mawazo ya vijana wa Kitanzania kukua kutoka ubunifu wa darasani hadi kuwa bidhaa zinazochangia maendeleo ya taifa, kuzalisha ajira na kuongeza ushindani wa uchumi unaotegemea maarifa.
Matokeo ya uwekezaji huo tayari yanaonekana. Mwaka 2025, Ekima Interactive ilishirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) kuzindua mfumo wa kujifunzia kidijitali unaotumika katika zaidi ya shule 2,000 za serikali, ukiwafikia maelfu ya walimu na wanafunzi nchini.
Kuenea kwa SmartDarasa katika shule hizo ni ushahidi kuwa uwekezaji wa Serikali kupitia COSTECH hauishii kutoa ruzuku kwa wabunifu, bali huzaa matokeo yanayowanufaisha wananchi moja kwa moja.
Walimu wamepata mbinu bora za kufundisha, wanafunzi wameongeza uelewa wa sayansi kwa vitendo na taifa limepata teknolojia ya ndani inayopunguza utegemezi wa suluhisho kutoka nje ya nchi.
Aidha, Ekima imeendelea kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania, Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) pamoja na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima katika kupanua matumizi ya teknolojia za kidijitali.
Kaimu Naibu Mkuu wa Taasisi Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Profesa Sempheo Siafu, anasema Ekima imeongeza upatikanaji wa elimu kwa kutumia TEHAMA, imeboresha mbinu za ufundishaji na kuleta unyumbufu wa kujifunza.
Kwa upande wake, Mwalimu kutoka Shule ya Sekondari Kilakala Morogoro,  Frank Asubisye anasema matumizi ya teknolojia hiyo yamebadili namna anavyofundisha. Kupitia video na maabara za kidijitali, wanafunzi wanaweza kuona kwa vitendo jinsi mwanga unavyopinda au kufanya majaribio ya Sheria ya Ohm na kuona matokeo kwa wakati halisi, jambo linaloongeza uelewa na uwezo wa kutumia maarifa hayo katika maisha halisi.
Mwanzilishi mwenza wa SmartDarasa, Kusiluka Aginiwe, anaamini bado kuna fursa kubwa ya kuifikisha teknolojia hiyo katika shule nyingi zaidi, hasa maeneo yenye changamoto ya maabara.
Anasisitiza ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wananufaika na elimu bora ya sayansi.
Safari ya SmartDarasa ni ushahidi kwamba mafanikio ya miaka 40 ya COSTECH hayaonekani katika takwimu pekee, bali katika maisha ya wananchi.
Kutoka wazo la kijana wa Kitanzania hadi teknolojia inayotumiwa katika maelfu ya shule, SmartDarasa inaonyesha kuwa uwekezaji wa Serikali katika sayansi, teknolojia na ubunifu unaweza kubadili changamoto kuwa fursa za maendeleo.
Kadiri Tanzania inavyoendelea kuwekeza katika wabunifu wa ndani, ndivyo inavyojenga uchumi unaotegemea maarifa, kuibua ajira, kuboresha huduma za jamii na kuimarisha ustawi wa Taifa. SmartDarasa ni mfano hai unaodhihirisha kuwa safari ya miaka 40 ya COSTECH imeweka msingi imara wa Tanzania inayotumia sayansi, teknolojia na ubunifu kama injini ya maendeleo endelevu.
Na Matokeo ya uwekezaji huo tayari yanaonekana. Mwaka jana  2025, Ekima Interactive ilishirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) kuzindua mfumo wa kujifunzia kidijitali unaotumika katika zaidi ya shule 2,000 za serikali, ukiwafikia maelfu ya walimu na wanafunzi nchini.
Kuenea kwa SmartDarasa katika shule hizo ni ushahidi kwamba uwekezaji wa Serikali kupitia COSTECH hauishii kutoa ruzuku kwa wabunifu, bali huzaa matokeo yanayoboresha maisha ya wananchi.
Walimu wamepata mbinu bunifu za kufundisha, wanafunzi wameongeza uelewa wa sayansi kwa vitendo, na taifa limepata teknolojia ya ndani inayopunguza utegemezi wa suluhisho kutoka nje ya nchi.
Aidha, Ekima Interactive imeendelea kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) katika kupanua matumizi ya teknolojia za kidijitali kwenye sekta ya elimu.
Kaimu Naibu Mkuu wa Taasisi Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu katika TEWW, Profesa Sempheo Siafu, anasema matumizi ya Ekima yameongeza upatikanaji wa elimu kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), yameboresha mbinu za ufundishaji na kuleta unyumbufu wa kujifunza kwa makundi mbalimbali ya wananchi.
Kwa upande wake, Mwalimu Frank Asubisye anasema matumizi ya teknolojia hiyo yamebadili kabisa namna ya kufundisha sayansi darasani.
“Teknolojia imelifanya darasa kuwa la ushirikishwaji zaidi. Badala ya mwanafunzi kusikiliza maelezo pekee, sasa anaona, anafanya majaribio na kuelewa kwa vitendo,” anasema.
Anatoa mfano wa mada ya mwanga kupinda ambapo wanafunzi hutumia video na vielelezo vya kidijitali kuona namna mwanga unavyobadilisha mwelekeo.
Vivyo hivyo, katika somo la Sheria ya Ohm, wanafunzi hufanya majaribio kupitia maabara za kidijitali na kuona uhusiano kati ya volti, mkondo wa umeme na ukinzani kwa wakati halisi.
Hali hiyo huongeza uelewa wa somo na kuwajengea uwezo wa kutumia maarifa hayo katika ubunifu wa vifaa vya kielektroniki na utatuzi wa changamoto mbalimbali.
Mbali na kuboresha elimu, SmartDarasa imefungua fursa mpya za ajira kwa wataalamu wa programu, wabunifu wa maudhui ya kidijitali, walimu na wataalamu wa teknolojia ya elimu.
Hivyo, ubunifu huo unaonyesha jinsi sayansi na teknolojia vinavyoweza kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi unaotegemea maarifa na kuongeza ushindani wa bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini.
Mwanzilishi mwenza wa SmartDarasa, Kusiluka Aginiwe, anasema bado kuna nafasi kubwa ya kuifikisha teknolojia hiyo katika shule nyingi zaidi, hasa zilizoko maeneo ya vijijini zenye changamoto ya maabara.
Anatoa wito kwa Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kuendelea kuwekeza katika ubunifu wa ndani ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike na elimu bora ya sayansi.
Kwa mtazamo mpana, SmartDarasa si hadithi ya mafanikio ya kampuni moja pekee. Ni kielelezo cha matokeo ya mfumo ambao COSTECH imeujenga kwa zaidi ya miaka 40 wa kutambua vipaji, kuviendeleza kupitia tafiti, kuvilea kwenye vituo vya uatamiaji wa biashara za teknolojia na kuvifikisha sokoni.
Katika kipindi hicho, COSTECH imeendelea kuwa daraja kati ya tafiti, wabunifu, vyuo vikuu, sekta binafsi na Serikali, hatua iliyowezesha mawazo ya Watanzania kubadilika kuwa bidhaa na huduma zinazotatua changamoto katika elimu, afya, kilimo, mazingira na sekta nyingine muhimu za maendeleo.
Safari ya SmartDarasa inaonyesha wazi kuwa uwekezaji wa Serikali katika sayansi, teknolojia na ubunifu si matumizi ya kawaida, bali ni uwekezaji unaozalisha matokeo ya muda mrefu kwa taifa. Kila fedha inayowekezwa katika wabunifu wa ndani huongeza uwezo wa Tanzania kujitegemea kiteknolojia, kuzalisha ajira, kuimarisha uchumi na kuboresha huduma kwa wananchi.
Katika maadhimisho ya miaka 40 ya COSTECH, SmartDarasa inasimama kama ushahidi hai wa mafanikio ya safari hiyo.
Kutoka katika wazo la mwanafunzi hadi kuwa teknolojia inayotumiwa katika zaidi ya shule 2,000 za serikali, ubunifu huu unaonyesha kuwa mazingira sahihi ya uwekezaji katika sayansi, teknolojia na ubunifu yanaweza kubadili changamoto kuwa fursa na kuifanya Tanzania kuwa taifa linalotegemea maarifa katika kufikia maendeleo endelevu.

You Might Also Like

Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo

Utafiti wa Chakula Bora cha Kuku wa Nyama Watoa Tumaini kwa Wafugaji

Kila Parachichi, Ndizi au Chungwa Ninalouza ni Tiketi Ya Matumaini Ya Watoto Wangu – Beatrice

REA Yajivunia Mafaniko ya usambazji wa Teknolojia za Nishati Safi kwa Wananchi Vijijini

Daraja La Magufuli Laimarisha Uhusiano Wa Jumuiya Ya China,Tanzania Yenye Mustakabali Wa Pamoja

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TVLA Yazalisha Chanjo ya Kudhibiti Homa ya Kutupa Mimba kwa Mifugo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TVLA Yazalisha Chanjo ya Kudhibiti Homa ya Kutupa Mimba kwa Mifugo
Habari August 1, 2026
Halmashauri Ya Jiji La Dodoma Lawataka Wakulima Kutumia Nanenane Kujifunza Kilimo Cha Kisasa
Habari August 1, 2026
Dkt. Nchemba: TPHPA Yazidi Kuwafikia Wakulima
Habari August 1, 2026
BRELA Kutumia Maonesho Ya Nanenane Kutoa Huduma Kuhusu Mfumo Ulioboreshwa
Habari August 1, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?