Na Lucy Lyatuu,Dodoma
KATIKA Kuadhimisha miaka 10 tangu kuanza kwa hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) iliyoko mkoani Dodoma, imepanga kurudisha tabasamu kwa wagonjwa wa Figo na uloto, wasiokuwa na uwezo ambapo inaitaka jamii kuchangia mfuko wa upandikizaji magonjwa hayo ili wagonjwa wapatiwe huduma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa BMH, Dkt Abdallah Baja amesema hayo wakati wahariri wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) walipofanya ziara katika hospitali hiyo kujionea huduma bobezi na za kibingwa zitolewazo hapo.

Akizungumza amesema gharama za matibabu kwa magonjwa hayo ni kubwa, na ili kupanua huduma hizo kwa wasiokuwa na uwezo yapasa wananchi kuchangia mfuko huo kuwezesha wahitaji kupata huduma.
Amesema kwa gharama za kupandikiza uloto hospitalini hapo ni sh milioni 75 kwa mgonjwa mmoja huku upandikizaji wa Figo ukigharimu sh milioni 45, gharama ambayo wananchi wa kawaida ni ngumu kuzifikia lakini kwa kuchangia mfuko huo utawezesha wengi kufikiwa na huduma.

Alitaja namnamya kuchangia mfuko huo kuwa ni kwa kutuma fedha kupitia namba986930000001 BMH Organ, na wagonjwamwataweza kufikiwa na huduma hiyo


