MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TARURA Yatenga Milioni 580 Kuboresha Barabara Zinazohudumia Sekta ya Madini Geita
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TARURA Yatenga Milioni 580 Kuboresha Barabara Zinazohudumia Sekta ya Madini Geita
Habari

TARURA Yatenga Milioni 580 Kuboresha Barabara Zinazohudumia Sekta ya Madini Geita

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
GEITA: WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), imetenga Sh milioni 580 kukamilisha barabara za kilomita 210, hasa zinazohusiana na shughuli za madini.
Meneja wa TARURA mkoa wa Geita,  David Msechu amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya nane ya sekta ya madini yanayoendelea mkoani Geita
Amesema fedha hizo zimetengwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 hadi 2025/2026, na kwamba hadi sasa baadhi ya kazi zimekamilika huku nyingine zikiendelea kutekelezwa.
Habari Picha 9597
Amesema TARURA wapo katika maonesho hayo ili kutoa elimu kwa umma kuhusu kazi wanazofanya katika kusimamia mtandao wa barabara za wilaya nchini.
Amesema taasisi hiyo inasimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara zenye jumla ya kilomita 100,044 nchi nzima, ambapo Geita pekee ina kilomita 7,264 na asilimia 60 ya mtandao huo unapitika. Kati ya hizo, kilomita 564 zinahudumia maeneo ya shughuli za madini.
Pia amesema TARURA inajivunia maabara ya kisasa inayopima ubora wa barabara na kazi nyingine za ujenzi.
Kwamba, maabara ya Geita imesaidia miradi mbalimbali kama ule wa umwagiliaji Ibanda, kituo cha umeme Nakayazi (TANESCO), na miradi ya
Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), na Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu kwa Ajili ya Ustawi wa Jamii na Ustahimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi (TACIP).
Habari Picha 9598
Aidha, TARURA Geita inatekeleza ujenzi wa madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe, ambapo tayari madaraja manne yamekamilika. Teknolojia hiyo inalenga kuongeza ubora na kupunguza gharama.
Amesema changamoto kubwa inayokabili barabara za maeneo ya madini ni magari makubwa kupita kwenye barabara zisizokidhi uzito zaidi ya tani 10.
Hivyo amesema wakala huo unatoa wito kwa wananchi na wawekezaji kushirikiana ili kuhakikisha barabara hizo zinaboreshwa kwa manufaa ya wote.
Habari Picha 9596
Kwa upande wake, Mhandisi Faiza Mbange kutoka makao makuu ya TARURA amesema wapo kwenye maonesho kutoa elimu kwa jamii juu ya matumizi sahihi ya barabara, kulinda miundombinu, na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala ya fidia kwa maeneo ya miradi.
Kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia, TARURA inatarajia kujenga kilomita 59 za barabara katika wilaya ya Mbongwe mkoani Geita, ambapo usanifu wa barabara tatu tayari umekamilika na hatua ya kumpata mkandarasi inaendelea.

You Might Also Like

Walimu Kupatiwa Mafunzo ya Tehama

DC Twange Apongeza Wananchi Kuchangia Maendeleo 

CCCC Yakutana na Wanahabari, Yapanga Mikakati Mipya 2025

Kilimo Shadidi Kinapunguza Uzalishaji Wa Gesi

Tanzania, Japan Kushirikiana Ukuzaji Ujuzi Kwa Vijana

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kingalame Asisitiza Umuhimu wa Wachimbaji Kuuza Dhahabu Serikalini
Next Article Kingalame Aitaka Sekta Binafsi Kushirikiana na TBA Kukamilisha Mradi wa Makazi Geita
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

ARTICLE 19,  JOWUTA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WANAHABARI
Habari October 18, 2025
Profesa Ndunguru Aongoza Kikao Cha Mawaziri Wa DLCO- EA Akimwakilisha Bashe
Habari October 17, 2025
Mgombea NCCR-Mageuzi Awaasa Watanzania Wasikubali Propaganda
Habari October 17, 2025
Profesa Nombo: Ushirikiano wa VETA, Sekta Binafsi Waimarisha Mafunzo ya Ufundi Stadi
Habari October 17, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?