MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: CCCC Yagusa Wanafunzi Msasani kwa Msaada wa Vifaa vya Shule, Chakula
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > CCCC Yagusa Wanafunzi Msasani kwa Msaada wa Vifaa vya Shule, Chakula
Habari

CCCC Yagusa Wanafunzi Msasani kwa Msaada wa Vifaa vya Shule, Chakula

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: KAMPUNI ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China (CCCC), imetoa msaada wa vifaa vya shule pamoja na chakula katika Shule ya Msingi ya Msasani A, iliyopo Dar es Salaam.
Kiongozi wa tawi la kampuni hiyo hapa nchini,  Deng Honglong amesema hayo wakati wa kukabidhi vifaa hivyo katika hafla iliyofanyika katika shule hiyo.
Habari Picha 9203
Amesema kampuni hiyo haijajikita pekee katika ujenzi wa miundombinu, bali pia katika kujenga mahusiano  yanayovuka mipaka ya lugha na mataifa, kwa lengo la kusaidia maendeleo ya kijamii, hususan ya watoto.
Amesema, ” Ninaposimama kwenye ardhi hii ya Tanzania, nikiwaangalia watoto walioko mbele yangu, moyo wangu hujaa upendo lakini pia mzigo wa kuwajali.
“Najua kuwa katika pembe mbalimbali ambazo hatuwezi kuziona, wapo watoto wengi wanaopambana na changamoto za maisha wengine hutembea kilomita kadhaa kwenda shule, wakiwa na vitabu vilivyochakaa na penseli zilizobaki vipande,”.
Amesema CCCC kwa miaka mingi imekuwa ikijenga barabara, bandari na reli, lakini mafanikio makubwa zaidi kwao ni kuunganisha watu kwa moyo wa utu kama ilivyo kwa falsafa ya “Ujamaa” ya Tanzania.
Habari Picha 9211
Katika tukio hilo CCCC ilitoa vifaa mbalimbali kwa watoto yakiwemo mabegi, kompasi, madaftari na vitabu mbalimbali kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Pia mipira, mchele, unga, mafuta ya kupikia ba zawadi nyingine nyingi.
“Tunatumaini kuwa watoto hawa watapitia vitabu hivi, kucheza kwa furaha, kula kwa kushiba, na zaidi ya yote, wajue kuwa dunia inawajali,” amesema.
Pia qmesema  msaada huo hauishii kwenye vifaa tu, bali ni ishara ya urafiki wa kweli na dhamira ya kulinda ndoto za watoto wa Kitanzania.
“Nguvu ya kampuni haipimwi kwa idadi ya majengo au barabara iliyojenga, bali kwa kile inachofanya kwa watu wa nchi husika hususan watoto wanaotegemewa kuwa viongozi wa kesho,” amesema.
Habari Picha 9206
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msasani A, Edward Mollel, ameishukuru CCCC kwa msaada huo mkubwa ambao umezidi matarajio yao.
“Tulipowasiliana nao, tuliomba madaftari na vitabu  vya kujifunzia, lakini wametuletea vitu vingi zaidi mabegi, mipira, mashine ya ‘photocopy’ na hata chakula. Tunashukuru sana,” amesema Mollel.
Qmewaomba wafadhili hao kusaidia kuboresha maktaba ya shule hiyo iwapo watapata fursa nyingine ya kushiriki.
Nao baadhi ya wanafunzi waliofaidika na msaada huo walieleza furaha yao, wakisema kuwa msaada huo utachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira yao ya kujifunza na kuleta matumaini kwa ndoto zao za baadaye.
Habari Picha 9212

You Might Also Like

Uvuvi Wa Kisasa Wainua Mwanza Kiuchumi

Jeshi la polisi kuchukua tahadhari mechi ya Simba, Yanga leo

Jaji Mwambegele: Habari Sahihi ni Msingi wa Ushiriki Mpana wa Wananchi Kura 2025

UDOM Yatumia Akili Mnemba Kugundua Dawa

Serikali Kuendelea Kuboresha Sheria za Ulinzi wa Watoto

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tanzania Kuweka Muongozo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Takwimu Kidijitali
Next Article Roman Glorig Ahuisha Mkataba wa Uwakilishi wa Heshima wa Tanzania Nchini Czech
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CHAUMMA Kuunda Mamlaka ya Mazao ya Kimkakati – Salum Mwalim
Habari September 14, 2025
Heshima ya Udaktari Ni Mwito wa Kulitumikia Taifa: Dkt Ikomba
Habari September 14, 2025
Rais Wa CWT Suleiman Ikomba Sasa Ni Daktari
Habari September 13, 2025
Salum Mwalim: Nitarejesha Hadhi ya Kanda ya Ziwa na Kuinua Zao la Pamba
Habari September 12, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?