MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Shinyanga Kunufaika Na Miradi Ya REA,Wauziwa Mitungi 13,000 Kwa Ruzuku
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Shinyanga Kunufaika Na Miradi Ya REA,Wauziwa Mitungi 13,000 Kwa Ruzuku
Habari

Shinyanga Kunufaika Na Miradi Ya REA,Wauziwa Mitungi 13,000 Kwa Ruzuku

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umeitambulisha kampuni ya Lake Gas Limited ambayo imepewa jukumu la kusambaza mitungi ya gesi 13,020 itakayouzwa kwa bei ya ruzuku ya asilimia 50 katika Mkoa wa Shinyanga.
Hayo yamebainishwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mhandisi wa Miradi kutoka REA,  Annet Ndyanabo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji mitungi ya gesi yenye ujazo wa kilo sita mkoani humo.
Ndyanabo amesema kuwa mitungi ya gesi 13,020 itakayosambazwa mkoani Shinyanga ni utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia ambao una lengo la kuongeza matumizi ya nishati safi kufikia asilimia 80 ifikapo 2034.
“Utekelezaji wa mradi huu unaenda sambamba na malengo ya Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia (2024-2034) ambao unalenga kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia kufikia asilimia 80 ya watanzania wanaotumia nishati hiyo ifikapo mwaka 2034,” Amesema  Ndyanabo.
Ameongeza kuwa, lengo la mradi ni kuongeza upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia kwa kuwawezesha wananchi wengi kumudu gharama za bidhaa za nishati safi  ili kutunza mazingira.
“Mradi huu utapunguza umaskini kwa kuwapa muda zaidi wanawake kushiriki katika shughuli za kiuchumi pindi wanapotumia mitungi ya gesi kama njia mbadala ya kupikia badala ya kuni na mkaa,” Ameongeza  Ndyanabo.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga,  Salum Hamduni ameipongeza REA kwa kuja na mradi huo na kuiomba iwe endelevu ili iweze kuwasambazia wananchi wengi nishati hiyo muhimu.
Naye, Mratibu wa nishati safi kutoka kampuni ya Lake Gas Limited, Ramadhan Siasa amesema watatekeleza mradi huo kwa kuzingatia makubaliano ya Mkataba wa kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia pamoja na kutoa elimu kwa wananchi ili kuchochea matumizi ya nishati hiyo.
Gharama ya Mradi huo ni sh 272,769,000 na wilaya zitakazonufaika ni pamoja na Wilaya ya  Shinyanga, Kishapu, Ushetu na Msalala na kila wilaya itapata mitungi 3,255.

You Might Also Like

Mongela Ajiridhisha Ushindi wa Kishindo , Uchaguzi Serikali za Mitaa,Uchaguzi Mkuu CCM

NIT Yajivunia Uanzishwaji Chuo Cha Marubani

Masauni: Mapendekezo Ya Kulifanya NEMC Kuwa Mamlaka Yamepokelewa

SPIKA asisitiza matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 

SEforALL Kuimarisha Ushirikiano Upatikanaji Nishati Endelevu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article SUA Chatumia Ngamia Mafunzo Ya Vitendo Kwa Wanafunzi
Next Article Ushiriki Wa Tanzania Jukwaa La Dunia Waongeza Fursa Za Kimataifa Kukabiliana Na Maafa-Dk Yonaz
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Viongozi Bora Hujenga Mazingira Wezeshi Kwa Wahadhiri – Profesa Nombo
Habari June 5, 2025
Sheria Ya Kupata  Taarifa, Ya NGOs Zina Upungufu 
Habari June 4, 2025
Mchengerwa Awafunda Walimu
Habari June 4, 2025
Ushiriki Wa Tanzania Jukwaa La Dunia Waongeza Fursa Za Kimataifa Kukabiliana Na Maafa-Dk Yonaz
Habari June 3, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?