MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ziwa Ngozi Lavuta Mamia Sabasaba, Wageni Washangazwa Na Ramani Ya Afrika Juu Ya Mlima
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ziwa Ngozi Lavuta Mamia Sabasaba, Wageni Washangazwa Na Ramani Ya Afrika Juu Ya Mlima
Habari

Ziwa Ngozi Lavuta Mamia Sabasaba, Wageni Washangazwa Na Ramani Ya Afrika Juu Ya Mlima

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu
WAGENI wanaotembelea banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) wameendelea kuvutiwa na simulizi kuhusu Ziwa Ngozi, moja ya vivutio vya kipekee vya utalii nchini, kinachopatikana ndani ya Hifadhi ya Mazingira ya Msitu wa Mlima Rungwe mkoani Mbeya.
Mvuto huo umechangiwa na maelezo yanayotolewa na Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira ya Msitu wa Mlima Rungwe, Jesca Mgata (pichani) ambaye amekuwa akiwafafanulia wageni historia, maajabu na upekee wa ziwa hilo linalotajwa kuwa la pili kwa ukubwa miongoni mwa maziwa ya kreta barani Afrika.
Akiwa katika banda la TFS, Jesca Mgata amesema wengi wanaofika kushuhudia maonesho hushangazwa wanapoelezwa kuwa Tanzania ina hazina kubwa ya vivutio vya utalii ambavyo bado havijafahamika vya kutosha, huku Ziwa Ngozi likiwa miongoni mwa vivutio vinavyozidi kupata umaarufu.
“Baadhi ya wageni hawaamini wanapoona picha za ziwa hili. Tunawaeleza kuwa liko juu ya mlima, limezungukwa na msitu mnene na limetokana na mlipuko wa volkano. Wengi huamua kulitembelea mara baada ya kupata taarifa hizi,” alisema.
Habari Picha 12753
Alieleza kuwa moja ya maajabu makubwa ya Ziwa Ngozi ni uwezo wake wa kuakisi umbo linalofanana na ramani ya Bara la Afrika, likiwa na mwonekano unaoonesha pande za kusini, mashariki, magharibi na kaskazini pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, jambo linalowavutia watafiti, wapiga picha na watalii kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Jesca Mgata, ziwa hilo linapatikana katika Milima ya Uporoto ndani ya Hifadhi ya Mazingira ya Msitu wa Mlima Rungwe na ni ziwa la kreta lililotokana na shughuli za volkano, tofauti na maziwa mengine makubwa ya asili. Ziwa hilo lina urefu wa takribani kilomita 2.5, upana wa kilomita 1.5, kina cha mita 74 na eneo la zaidi ya hekta 9,332.
Alisema mazingira ya ziwa hilo yanatoa fursa za utalii wa ikolojia, matembezi ya milimani, utazamaji wa ndege, upigaji picha na tafiti za kijiolojia, huku mandhari yake ya kipekee yakiendelea kuwavutia wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mgata alibainisha kuwa TFS inaendelea kutumia Maonesho ya Sabasaba kutangaza vivutio vilivyopo kwenye hifadhi za misitu ili kuongeza idadi ya watalii wa ndani na wa kimataifa, akisisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kujivunia na kutembelea hazina zao za asili.
Katika maonesho hayo, banda la TFS limeendelea kupokea maelfu ya wageni wanaojifunza kuhusu utalii wa misitu, uhifadhi wa mazingira na vivutio vya kipekee vinavyopatikana nchini, huku simulizi za Ziwa Ngozi zikizidi kuhamasisha wengi kupanga safari ya kutembelea Hifadhi ya Mazingira ya Msitu wa Mlima Rungwe.

You Might Also Like

AU yataka vyombo vya habari Afrika, kulinda Uhuru wa vyombo vya habari 

Rita Kabati Aahidi Kuimarisha Miundombinu, Kuwatumikia Wananchi Wa Kilolo

Mbarawa Aitaka Jamii Kulinda Miundombinu ya Uchukuzi

Sera mpya ya viwanda kuzinduliwa

Mchengerwa Awafunda Walimu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Shirika La Uzalishaji Mali La Polisi Kujenga Vituo Vya Ukaguzi Wa Vyombo Vya Moto
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Shirika La Uzalishaji Mali La Polisi Kujenga Vituo Vya Ukaguzi Wa Vyombo Vya Moto
Habari July 9, 2026
Watumishi 7881 Watakaostaafu 2026/27 Watambuliwa Kupitia Kampeni Ya Tunalipa Jana-PSSF
Uncategorized July 8, 2026
Katambi Apongeza Zimamoto Kwa Uwekezaji Wa Vifaa Vya Kisasa
Uncategorized July 7, 2026
Uwekezaji wa Vijana Watajwa Chachu ya Ukuaji wa Uchumi
Habari June 29, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?