MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Washauriwa Kutumia Mbegu Zinazokabiliana Na Mabadiliko Ya Tabia Nchi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Washauriwa Kutumia Mbegu Zinazokabiliana Na Mabadiliko Ya Tabia Nchi
Habari

Washauriwa Kutumia Mbegu Zinazokabiliana Na Mabadiliko Ya Tabia Nchi

Author
By Author
Share
4 Min Read
Mwandishi wetu
ARUSHA: WAKULIMA wa mazao mbalimbali ikiwepo mbogamboga na matunda nchini, wametakiwa kutumia mbegu bora  zinazoweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi .
Hivi sasa Ongezeko la joto ardhini katika maeneo mengi nchini linalosababisha  mbegu za mazao na mazao yaliyopandwa kuharibika na kushindwa kutoa mazao bora.
Mtaalam wa sayansi ya mimea wa kampuni ya Balton Tanzania, Chonya Wema akizungumza katika siku ya wakulima ya maonesho ya mbegu jijini Arusha, ambayo huandaliwa kila mwaka na kampuni hiyo, amesema kampuni hiyo imeanza kuzalisha mbegu zinazokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Wema amewataka wakulima kutumia mbegu  hizo kwa kuzingatia ushauri wa wataalam wa mimea ili kunufaika na kilimo na kuongeza uzalishaji.
Amesema  hivi sasa kuna aina nyingi ya mbegu lakini baadhi ya hizo mbegu haziwezi kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa hivyo kushambuliwa na wadudu wa mimea kwa urahisi na kumpatia hasara mkulima.
“Kama ambavyo mnaona hili shamba darasa mazao yamekuwa vizuri kutokana na matumizi ya mbegu bora na pembejeo nzuri,” amesema.
Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya udhibiti wa mbolea ,Gothad Liampawe amesema, mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwani ni kipindi cha kilimo .
Amesema mamlaka hiyo imejitahidi kudhibiti uingizwaji wa mbolea feki ili kumkwamua mkulima na athari za matumizi ya mbolea zisizo na ubora.
“Udhibiti wa mbolea uko vizuri kwani serikali imetoa ruzuku kwa mbolea ambapo mkulima aliyejisajili kwa ngazi ya Kijiji anapatiwa mbolea ya ruzuku,” amesema.
Baadhi ya wakulima na wauzaji wa pembejeo wakizungumza katika maonesho hayo walipongeza a kampuni ya BALTON Tanzania ambao ni waagizaji na wasambazaji wa mbegu nchini.
Saidi Bakari Hamza kutoka Pemba na Masudi Salimu Nasoro kutoka Unguja wamesema wamejifunza  kutambua mbegu bora kulingana na maeneo waliyotoka na kuahidi kwenda kutoa ushauri kwa wakulima wa maeneo yao.
‘’Kumekua na changamoto kwa wakulima tunaowahudumia kule pemba pindi unapowauzia mbegu waliyohitaji
Meneja mkuu wa kampuni ya Balton Tanzania Jacob vorster  amesema waliamua kuwaita wakulima hao na wasambaji wa mbegu katika mafunzo hayo ili kuongeza ujuzi wa mbegu na kilimo.
Amesema wanataka kuona kilimo.ambacho kina tija katika maeneo yao na kufanikisha malengo ya mkulima kupata mazao mengi na bora baada ya kutumia mbegu bora.
Amesema kufanya kilimo chenye tija katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia nchi kutapelekea nchi kuwa na chakula cha kutosha na pia kuongeza kipato cha mkulima mmoja mmoja.
Awali akifungua maonesho hayo,Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa uzalishaji na usambazaji wa mbegu nchini (TASTA) Bobu Shuma amewataka wakulima na wauzaji mbegu kushirikiana.
Amesema wakulima  wanatakiwa kupata ushauri wa mbegu bora inayofaa kulingana na mahali wanapolima kuendana na mazingira ya hali ya hewa.
“Lazima wauzaji ña mbegu mshirikiane na wakulima ili muwasaidie   kupata mazao bora na kuepuka hasara ya kutumia mbegu zisizo na ubora,” amesema.
Wakulima na mawakala.wa pembejeo zaidi ya 400 wameshiriki katika maonesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka.

You Might Also Like

JMAT Yatoa Neno Yanayoendelea Kwa Vijana Wa Kenya

TARURA Yaunganisha Vijiji Vya Ifinisi, Kambanga na Bugwe Wilayani Tanganyika

TPHPA Yaelezea Vipaumbele Vyake

Wataalam wa “Visit Finland” Wabadilishana Uzoefu Kutangaza Utalii Duniani 

Trump Ashinda Uchaguzi Marekani

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Nyamhokya: Mei Mosi Ni Singida Mwaka Huu 2025
Next Article Ukusanyaji Mapato Halmashauri Hauridhishi – Ndugange
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?