Ridhiwani Aihakikishia Uwekezaji Endelevu
Na Lucy Ngowi
KILIMANJARO: KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), imepongeza serikali kwa uwekezaji wenye tija na manufaa kwa maendeleo ya nchi katika kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za ngozi Kilimanjaro International Leather Industries Co Ltd.
Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho, Mwenyekiti wa kamati hiyo Agustine Holle amesema uwekezaji waliouona utaiwezesha serikali kuongeza mapato.
Pia amesema kiwanda hicho kitaunufaisha mkoa wa Kilimanjaro pamoja na mikoa ya jirani kwa kuboresha mfumo wa maisha na kuongeza kipato kwa wakazi wake.
Amesema kiwanda hicho kitakapokamolika kitatoa ajira 3000 za moja kwa moja, nyingine zisizo za moja kwa moja 4000.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema ataendelea kusimamia maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuufanya uwekezaji huo unakuwa endelevu kwa manufaa ya watanzania na nchi.
