MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ajiandikisha Kijijijni Nandagala
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ajiandikisha Kijijijni Nandagala
Habari

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ajiandikisha Kijijijni Nandagala

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amejiandikisha katika Daftari la Mpigakura kwa ajili ya kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.
Majaliwa ambaye alifuatana na mkewe Mary Majaliwa, amejiandikisha leo Jumamosi, Oktoba 19, 2024 kwenye Shule ya Msingi Nandagala iliyopo kitongoji cha Nanguruwe, Kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa pamoja na wanakijiji  wengine walifika kituoni hapo.
Akitoa taarifa ya uandikishaji, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ruangwa, Frank Chonya amesema wilaya ya Ruangwa ina tarafa tatu, kata 22, vijiji 90 na vitongoji 435 ambavyo vitahusika kwenye uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Vijiji.
Amesema wilaya hiyo imekadiria kuandikisha wakazi 123,803 ambapo kati yao 60,188 ni wanaume na 63,615 ni wanawake.
“Hadi kufikia Oktoba 18, 2024, tumefanikiwa kuandikisha jumla ya watu 103,468 ambapo kati yao wanaume ni 47,664 na wanawake ni 55,804,” amesema.
Amesema zoezi uandikishaji huo unaendelea hadi kesho Oktoba 20, 2024 saa 12 jioni.
Akizungumza na wananchi waliokuwepo kwenye kituo hicho, Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, amewashukuru viongozi wa Serikali za Vijiji wa Kata ya Nandagala kwa kuhamasisha watu wajitokeze kujiandikisha na kuifanya kata hiyo iwe ya kwanza kwa uandikishaji katika jimbo hilo.
“Kazi ya uandikishaji inaendelea nchi nzima na mwisho wa uandikishaji ni kesho. Tuwahimize wengine ambao bado hawajajiandikisha, nao pia waje kujiandikisha,,” amesema.

You Might Also Like

OUT Yawapiga Msasa Watumishi Wa Mamlaka Za Serikali Za Mitaa

TASU yaiomba serikali inunue kutoa ajira kwa mabaharia

Wafugaji huchakachua maziwa kwa kuongeza mafuta, maji, magadi au mkojo wa ng’ombe

Wakazi Wa Ntyuka Wataka Kiongozi Mchapakazi

USAID yatoa Dola mil nane Kwa kampuni za Tanzania

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ridhiwani Aongoza Majadiliano Ya Taarifa Ya Utekelezaji Wa Majukumu PSSSF
Next Article Masauni Akabidhi Polisi Magari 77
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbegu Bora za Miwa Zenye Tija ya Tani 200 kwa Hekta Zaendelea Kuwanufaisha Wakulima
Habari August 7, 2025
Mbegu Bora za Mpunga Zazalishwa TARI Dakawa, Ifakara
Habari August 7, 2025
Mtego wa Inzi Wa Matunda Suluhisho Salama kwa Wakulima
Habari August 7, 2025
Mafua, Kifua Yadaiwa Kusababisha Kifo cha Job Ndugai
Habari August 7, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?