MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Watumishi wa Umma Watakiwa Kuwa na Nidhamu, Ubunifu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Watumishi wa Umma Watakiwa Kuwa na Nidhamu, Ubunifu
Habari

Watumishi wa Umma Watakiwa Kuwa na Nidhamu, Ubunifu

Author
By Author
Share
3 Min Read
Pia Waajiri Watakiwa Kufanya Kazi Kwa Karibu Na Watumishi Kuepusha Migogoro
Na James Kamala, Ofisa Habari, Halmashauri ya Mji Nzega.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu amewataka watumishi wa umma kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii katika kuwahudumia wananchi ili kuleta tija kwa maendeleo ya taifa.
Aidha amewataka waajiri wote katika utumishi wa umma kuhakikisha wanafanya kazi kwa karibu na watumishi ili kuepusha migogoro isiyo na tija kwenye utumishi wa umma.
Sangu ameyasema hayo wakati akisikiliza na kutatua  kero mbalimbali zinazowakabili watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Tabora.
“Watumishi wa umma mnapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia nidhamu, ubunifu, kuboresha na kutathmini utendaji wenu ili wananchi waweze kupata matokeo chanya kwenye huduma wanazopatiwa,” amesema.
Amesema serikali imekuwa ikitenga na kutuma fedha za miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu na miundombinu, hivyo watumishi wa umma wanapaswa kuendana na kasi hiyo.
Kuhusu upungufu wa watumishi katika Halmashauri ya Mji wa Nzega na Mkoa wa Tabora,  Sangu amesema tatizo hilo tayari limepatiwa ufumbuzi kwani mchakato wa kuajiri watumishi tayari umeanza.
 “Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa vibali vya ajira mpya zaidi ya elfu arobaini na saba na tayari Mkoa wa Tabora unatarajia kupata watumishi wapya zaidi ya 4,000, tukianza na kada za afya,” amesema.
Kuhusu upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma, Naibu Waziri huyo amesema kuwa serikali imekwisha tenga fedha za kutosha kwa ajili ya mchakato huo, ikiwemo pia fedha za kulipa madeni mbalimbali  kama vile malimbikizo ya mishahara ya watumishi.
 Wakati huohuo, Sangu amewaasa waajiri kuhakikisha wanatoa mafunzo ya awali kazini kwa watumishi wapya ili waweze kujua wajibu wao na haki zao, na hivyo kuepusha migogoro kazini na mashauri ya kinidhamu katika maeneo ya kazi.
“Wajulisheni na kuwaelekeza mazingira ya kazi, kanuni, na sheria za utumishi wa umma ili waweze kufanya kazi kwa uhuru na amani yenye tija kwa utendaji uliotukuka,” amesema.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ricardo Komanya, pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, Leah Kibaki, na watumishi kutoka Idara na Vitengo mbalimbali katika Halmashauri hiyo.

You Might Also Like

UDSM  Kujenga Jengo La Kisasa La Bil 8.3

TARI Yawafikia Wakulima Kilosa, Kilimo Shadidi Cha Mpunga

Ruto: Diplomasia Itumike Kumaliza Mgogoro Kongo

Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan, kuongoza Kamati Kuu Maalum kesho

CCM yavunja rekodi – Makala

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Masauni Kuzifanyia Kazi Changamoto Alizozibaini Katika Ziara Yake
Next Article Polisi Dar yashikilia watatu kwa mauaji ya mfanyakazi wa Kampuni ya Hope Recycling
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?