MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mikataba ya zaidi ya bilioni 50 kuhamasisha nishati salama
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mikataba ya zaidi ya bilioni 50 kuhamasisha nishati salama
Habari

Mikataba ya zaidi ya bilioni 50 kuhamasisha nishati salama

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na Mwandishi Wetu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatarajia kusaini mikataba yenye thamani ya Sh.bilioni 50.98 kwa ajili ya kuhamasisha umma kuachana na matumizi ya nishati za kupikia zisizo salama.
Ihamasishaji huo ni hatua ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi za Kupikia.
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu kutoka REA) Advera Mwijage amesema hayo katika mkutano na Waandishi wa Habari Septemba 11, 2024 Jijini Dodoma.
Amesema utekelezaji wa miradi ya Nishati Safi na zilizoboreshwa za kupikia ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Nishati Safi 2024- 2034 ambao unaelekeza ifikapo Mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi za kupikia.
“Hivi karibuni, Wakala utasaini mikataba kadhaa ya ushirikiano na wadau mbalimbali ambayo yote kwa pamoja imelenga kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi za Kupikia kwa wote kama Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Nishati safi za Kupikia unavyoelekeza,,” amesema.
Amesema kwa upande wa Jeshi la Magereza, mikataba itakayosainiwa ina thamani ya sh bilioni 35.23 ambapo kati ya fedha hizo  asilimia 75.5 ambayo ni sawa na shi bilioni 26.57 zitatolewa na REA na asilimia 24.6 sawa na sh bilioni 8.66 zitatolewa na Jeshi la Magereza kwa Mradi utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitatu katika Magereza 129 yaliyopo Tanzania Bara.
“Katika mkataba huu na Magereza kazi zitakazofanyika ni pamoja na ujenzi wa mifumo ya bayogesi 126, usimikaji wa mifumo 64 ya gesi ya LPG, usimikaji wa mfumo wa gesi asilia,
“Pia usambazaji wa mitungi ya gesi (LPG) ya kilo 15 ikiwa na jiko la sahani mbili ipatayo 15,920 kwa watumishi wa Magereza, usambazaji wa tani 865 za mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe kutoka STAMICO,” amesema.
Amesema mkataba huo wa Magereza utahusisha pia usambazaji wa mashine 61 za kutengeneza mkaa mbadala, ujengaji uwezo kwa watumishi 280 wa Jeshi la Magereza na usambazaji wa majiko banifu 977.
Kati ya majiko hayo, 377 yatatumia nishati ya bayogesi, 256 yatatumia LPG na 344 yatatumia nishati ya mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe kwa kuanzia na baadaye kwa mkaa unaotokana na mabaki ya mazao mbalimbali.
Kwa upande wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), amesema mikataba itakayosainiwa ina thamani ya sh. bilioni 5.75 ambapo kati ya fedha hizo asilimua 76 ambayo ni sawa na sh. bilioni 4.36 itatolewa na REA na huku asilimia 24 sawa na sh. bilioni 1.39 itatolewa na JKT.
Amesema katika kuwezesha kaya za vijijini na zile zilizopo katika maeneo ya vijiji-miji kutumia nishati safi za kupikia na zilizoboreshwa, Serikali kupitia REA inaendelea kutoa ruzuku katika uuzaji wa wa mitungi ya gesi (LPG) ya Kilo 6.
Ametaja kampuni zilizoshinda zabuni ya kusambaza mitungi hiyo kuwa ni Taifa Gas, Manjis, Oryx pamoja na Lake Oil ambapo alisema mitungi 452,445 itasambazwa kwa bei ya ruzuku katika mikoa yote ya Tanzania Bara na huku kila wilaya ikinufaika na mitungi 3,255.

You Might Also Like

Askari wa Jeshi La Uhifadhi Kusini Wakumbushwa Wajibu

NIT yawapika vijana

Dkt. Tumbo Aitaka Jamii Kuelimishwa Namna Bora Ya Kuhifadhi Taka

Matumizi Holela Ya Vilevi Hatari Kwa Watumiaji

SUA Chatumia Ngamia Mafunzo Ya Vitendo Kwa Wanafunzi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Majaliwa Asema Sekta ya Uvuvi Yaingiza trilioni 2.9 kwa Mwaka 
Next Article Swahili International Tourism Expo Kufanyika Oktoba 11 hadi 13
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?