MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Jamii Yatakiwa Kuzungumza Pamoja Kuhusu Maji, Masuala ya Jinsia
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Jamii Yatakiwa Kuzungumza Pamoja Kuhusu Maji, Masuala ya Jinsia
Habari

Jamii Yatakiwa Kuzungumza Pamoja Kuhusu Maji, Masuala ya Jinsia

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi wetu
MOROGORO: JAMII imehamasishwa kushirikiana kushughulikia masuala ya maji na jinsia ili kufungua mlango wa uwezeshaji, usawa, na maendeleo endelevu katika upangaji na utekelezaji wa miradi na sera za Sekta ya Maji.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, ametoa wito huo mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa Mdahalo wa Wadau kuhusu Maji na Jinsia, ulioandaliwa na Wizara ya Maji kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji.
“Bila maji safi na salama, jamii haiwezi kustawi, uchumi hauwezi kukua, na mazingira hayawezi kuendelezwa. Hivyo kila mmoja ana jukumu la kuwa tayari kushirikiana,” amesema Waziri Kairuki.
Habari Picha 11511
Waziri huyo pia amesisitiza kuwa Serikali imeweka maji kuwa moja ya vipaumbele muhimu katika jitihada za kuboresha maisha ya wananchi kwa kuweka mikakati na kuimarisha uwekezaji katika sekta hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mwajuma Waziri, amesema Wizara imejipanga kuhakikisha inatoa majibu ya changamoto zinazowakumba wananchi wa jinsia zote katika upatikanaji wa majisafi na salama.
“Hali hii bado inaathiri makundi mbalimbali, hususan wanawake na wasichana ambao hubeba jukumu kubwa la kutafuta na kusimamia matumizi ya maji katika familia,” amesema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Jackson Kiswaga, amesema kamati yake ipo tayari kupokea na kuyafanyia kazi mapendekezo ya wadau.
“Kazi kubwa ya Bunge ni kutunga Sheria, kuisimamia Serikali, na kuwawakilisha wananchi. Tunategemea kupitia mdahalo huu kupata mapendekezo ya kuzingatia masuala ya kijinsia ipasavyo,” amesema.
Wiki ya Maji, inayoadhimishwa na Wizara ya Maji kuanzia leo Machi 16 hadi 22, mwaka huu 2026, inalenga kuongeza ufahamu juu ya umuhimu wa maji na kuhimiza ushirikiano wa kijamii katika usimamizi wa rasilimali hiyo muhimu.

You Might Also Like

Mikataba ya Bilioni 50.9 Yasainiwa kuwezesha nishati safi ya kupikia

Ridhiwani Kikwete Ajiandikisha Kupiga Kura Kijijini Msoga

Kima Cha Chini Cha Mshahara Chapanda Kwa Asilimia 35.1-Rais Samia

Samia ashiriki mashindano ya dunia ya Quran

Atoa Maelekezo Kwa Chuo Cha Hombolo Kuwajengea Uwezo Viongozi Wa Mitaa Na Vijiji -Kapinga

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tume Ya Madini Yaweka Vipaumbele Kuwezesha Vijana Kushiriki Katika Uchimbaji Madini 
Next Article Sh. Bilioni 883.93 Zatumika Kutekeleza Miradi ya Maji, Usafi wa Mazingira
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mwandishi Lucy Ngowi Miongoni mwa Waliong’ara Mei Mosi
Habari May 2, 2026
Tanzania yaendelea kuwa Shule ya Utumishi Barani Afrika,
Habari April 29, 2026
Wizara Ya Kilimo Yaomba Bunge Kuidhinisha Trilioni 1.1,Yaweka Mikakati Kuimarisha Sekta Hiyo
Habari April 28, 2026
NSSF Yafikia Trilioni 11.2, Hifadhi Skimu Yatajwa Kubadili Maisha ya Watanzania
Habari April 27, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?