MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Majaliwa Asema Sekta ya Uvuvi Yaingiza trilioni 2.9 kwa Mwaka 
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Majaliwa Asema Sekta ya Uvuvi Yaingiza trilioni 2.9 kwa Mwaka 
Habari

Majaliwa Asema Sekta ya Uvuvi Yaingiza trilioni 2.9 kwa Mwaka 

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema sekta ya uvuvi inaingiza mapato ya sh. trilioni 2.9 kwa mwaka, pia inakua kwa wastani wa asilimia 1.9 .
Majaliwa amesema hayo leo  Septemba 11, 2024 wakati akifungua Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (OACPS) wanaohusika na masuala ya Uvuvi, Bahari, Maziwa na Mito mkoani Dar es Salaam.
Amesema wastani wa uzalishaji wa samaki kwa mwaka nchini unafikia tani 472,579, huku tani 429,168 sawa na asilimia 91 zikitokana na uvuvi wa kawaida wa kutumia vyanzo vya asili ndani ya bahari, mito na maziwa na tani 43,411 sawa na asilimia tisa zikitokana na ufugaji wa samaki.
Akizungumza kwa niaba ya  Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu amesema kila siku watu 230,000 wanajishughulisha na uvuvi mdogo, Watanzania takriban milioni sita wamepata ajira zisizo za moja kwa moja kwenye sekta hiyo.
“Uvuvi mdogo mdogo unachangia zaidi ya asilimia 95 ya mavuno yote ya samaki nchini,” amesema.
Majaliwa amesema Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuendeleza sekta hiyo kutokana na rasilimali kubwa za maji ilizonazo ikiwa ni pamoja na Bahari ya Hindi, maziwa, mito, mabwawa mengi ya asili na yaliyojengwa na binadamu.
“Tanzania ina Eneo Maalum la Kiuchumi la kilomita za mraba 223,000, ambalo ni takriban asilimia 24 ya ardhi yote ya Tanzania.
“Hivi sasa, uvuvi wa kibiashara katika eneo hilo unafanywa hasa na Mataifa ya Uvuvi wa Maji ya Mbali chini ya mikataba ya leseni za uvuvi.
“Eneo Maalum la Kiuchumi la Tanzania ni fursa kubwa ya uwekezaji kupitia ununuzi wa meli za uvuvi, uwekezaji wa huduma za meli, usambazaji wa vifaa vya uvuvi, usambazaji wa chakula (maji, chakula na matunda), kuongeza thamani na usindikaji, utafiti na ulinzi wa baharini na angani.” amesema.
Amezitaja fursa nyingine za uwekezaji kuwa ni pamoja na uvuvi wa kina kirefu kwa ajili ya samaki aina ya tuna; kilimo cha mwani; uzalishaji wa vifaranga na chakula cha samaki.
Akielezea matarajio ya mkutano huo, Waziri Mkuu amesema mkutano huo utatoa mwongozo wa kimkakati kwenye vikao vya juu vya maamuzi vya Umoja wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki ili kuboresha usimamizi wa bahari, uvuvi na ufugaji endelevu wa samaki.

You Might Also Like

Kanzidata ya Taifa ya Uwekezaji Yalenga Kuboresha Takwimu na Kuvutia Wawekezaji

Dada wa kazi aliyejeruhi akamatwa

Mchome: Ubunifu wa VETA Ni Mkubwa, Sasa Ni Wakati Wa Uzalishaji Kwa Wingi

Ridhiwani: Maandalizi Mei Mosi  Yafikia Asilimia 88

Kanisa Lawashika Mkono Shule Ya Msingi Kibamba, Halmashauri Ya Ubungo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wasilisheni Migogoro Yenu Tume ya Usuluhishi na Uamuzi – Massawe
Next Article Mikataba ya zaidi ya bilioni 50 kuhamasisha nishati salama
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Bunge Marathon kufanyika April 18,yakidhi viwango vya kimataifa
Habari April 14, 2026
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu, Aongoza Harambee Mei Mosi 2026
Habari April 14, 2026
Ubunifu Wa Majengo Watakiwa Kuzingatia Tija Na Gharama Nafuu
Habari April 11, 2026
Waziri Ulega aridhishwa na miradi ya dharura TANROADS
Habari April 11, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?