MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TPHPA yawataka wakulima, wafanyabiashara kulinda ubora wa mazao, yafungua soko la viazi Zambia
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TPHPA yawataka wakulima, wafanyabiashara kulinda ubora wa mazao, yafungua soko la viazi Zambia
Habari

TPHPA yawataka wakulima, wafanyabiashara kulinda ubora wa mazao, yafungua soko la viazi Zambia

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imewataka wakulima kutumia viuatilifu vilivyosajiliwa kwa kufuata ushauri wa wataalamu, huku wafanyabiashara na wasafirishaji wakitakiwa kuhakikisha mazao yanakidhi viwango ili kuongeza ushindani wa Tanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Ndunguru, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Mamlaka kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na mwelekeo wa mwaka 2026/2027.
Profesa Ndunguru amesema wakulima wanapaswa kutoa taarifa mapema wanapoona wadudu au dalili zisizo za kawaida kwenye mazao, kushirikiana na Maofisa Ugani pamoja na wataalamu wa TPHPA na kuepuka matumizi holela ya viuatilifu, ambayo yanaweza kuhatarisha afya ya binadamu, mazingira na masoko.
Habari Picha 13475
Kwa wafanyabiashara na wasafirishaji, amesema ni muhimu kuzingatia taratibu za afya ya mimea na kuhakikisha mazao yanakidhi masharti ya nchi wanazokusudia kuuza, hatua itakayosaidia kupunguza changamoto ya mizigo kukataliwa katika masoko ya nje.
Aidha, TPHPA imesema inalenga kuongeza fursa za biashara ya viazi mviringo katika soko la Zambia kwa kusimika mtambo wa kusafishia viazi katika eneo la Makambako.
Hatua hiyo inalenga kuongeza ubora na ushindani wa zao hilo katika masoko ya nje.
Profesa Ndunguru amesema kilimo si uzalishaji pekee, bali ni fursa ya biashara na ajira, hususan kwa vijana, kupitia masoko yaliyofunguliwa na matumizi ya teknolojia za kisasa.
Habari Picha 13476
Katika mwaka wa fedha 2025/2026, Tanzania imefikia utoshelevu wa chakula wa asilimia 130, huku uzalishaji ukifikia tani 23,783,128.
TPHPA pia imedhibiti kwelea kwelea milioni 233.5 katika wilaya 21, hatua iliyosaidia kuokoa takribani tani 1,092,780 za nafaka, huku udhibiti wa viwavi jeshi katika Halmashauri 52 ukiokoa takribani tani 342,787.5 za mazao.
Habari Picha 13482
Habari Picha 13483
Habari Picha 13484

You Might Also Like

Wadau Wakaribishwa Kuwekeza Katika Uchakataji, Biashara ya Mkonge Nchini

Waziri wa Vijana akutana na Mwita wa Zanzibar

Makumbuli: Tunapinga kilimo cha bangi na mirungi

Mkongo Wa Mawasiliano Unalenga Kuleta Tija Kwa Wananchi

Muhogo, viazi kuongezewa tija kwenye uzalishaji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article PBPA Yashiriki Tamasha La Nne La Kitaifa La Utamaduni
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

PBPA Yashiriki Tamasha La Nne La Kitaifa La Utamaduni
Habari August 27, 2026
TFNC Yahimiza Wanaotoa Ushauri Wa Lishe Mitandaoni Kushirikiana Na Taasisi Zenye Mamlaka
Habari August 27, 2026
TaSUBa Yahimiza Vijana Kuzifikia Fursa Za Mafunzo Ya Sanàa Na Utamaduni
Habari August 27, 2026
Mfuko Wa Utamaduni Watoa Sh Bil 14.7 Kwa Miradi Ya Sanaa
Habari August 26, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?