MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading:  Wanasheria Wa TANESCO Watakiwa Kuendelea Kusimamia Maadili Na Taaluma-Twange
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari >  Wanasheria Wa TANESCO Watakiwa Kuendelea Kusimamia Maadili Na Taaluma-Twange
Habari

 Wanasheria Wa TANESCO Watakiwa Kuendelea Kusimamia Maadili Na Taaluma-Twange

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MKURUGENZI  Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),  Lazaro Twange, amewataka wanasheria wa shirika kuendelea kusimamia maadili ya taaluma, kutoa ushauri wa kisheria kwa wakati na kulinda maslahi ya shirika ili kuimarisha utendaji na kuhakikisha TANESCO inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
 Twange ameyasema hayo wakati akifungua Jukwaa la Wanasheria wa TANESCO lililoanza Julai 28, 2026 jijini Mwanza, likiwakutanisha wanasheria kutoka Makao Makuu, Ofisi za Kanda na Kampuni Tanzu za TANESCO kwa lengo la kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya kisheria yanayohusu utendaji wa shirika.
Habari Picha 12956
Akizungumza katika ufunguzi wa jukwaa hilo, Twange amewapongeza wanasheria hao kwa mchango wao katika kulinda maslahi ya shirika na kuhakikisha shughuli zake zinafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu.
“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya. Ushauri wa kisheria unaotolewa kwa wakati umekuwa ukisaidia TANESCO kufanya maamuzi sahihi na kuepusha migogoro ambayo ingeweza kuzuilika mapema,” amesema Twange.
Amewasisitiza kuendelea kuzingatia maadili ya taaluma, kutunza siri za kazi na kutoa ushauri wa kitaalamu unaolinda maslahi ya shirika.
“Kila mmoja wetu ana wajibu wa kulinda taasisi. Kwa upande wa wanasheria, hilo linaanza na kuzingatia maadili ya taaluma, kutunza siri za kazi na kuhakikisha kila ushauri unaotolewa unalinda maslahi ya TANESCO na kuimarisha utendaji wake,” amesema.
Habari Picha 12957
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa TANESCO, Wakili Sundi Mahalu, amesema idara hiyo itaendelea kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ili kuhakikisha shughuli za shirika zinaendelea kufanyika kwa kuzingatia misingi ya utawala bora na sheria.
“Jukwaa hili linatupa nafasi ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuimarisha uwezo wetu wa kitaaluma ili tuendelee kutoa huduma bora za kisheria zinazochangia mafanikio ya TANESCO,” amesema Wakili Mahalu.
Jukwaa la Wanasheria wa TANESCO linafanyika kwa siku tatu likiwa sehemu ya mkakati wa shirika wa kuendelea kuimarisha uwezo wa wataalamu wake wa sheria, hatua inayochangia ufanisi wa utendaji, usimamizi bora wa masuala ya kisheria na ulinzi wa maslahi ya shirika.

You Might Also Like

Wanafunzi 431, Watumishi 52 Watembelea TARI kujifunza Kilimo

Erio atoa elimu ya bidhaa bandia kwenye mabanda nanenane

Toleo La Sheria Zilizotafsiriwa Kwa Kiswahili Kutoka Agosti

Dkt. Nchimbi Azindua Mfumo Mpya wa Utabiri wa Kiasi cha Maji Morogoro

‎ ‎EWURA  Yatoa  Leseni Za Mafundi Umeme  Zaidi Ya 1000

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article WRRB Kuanza Kuingiza Sekta Ya Mifugo Kwenye Mfumo Wa Stakabadhi Za Ghala
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

WRRB Kuanza Kuingiza Sekta Ya Mifugo Kwenye Mfumo Wa Stakabadhi Za Ghala
Habari July 31, 2026
Wadau Wa Kilimo Iondoeni Nchi Kwenye Uchuuzi Wa Mafuta Ya Kula-Chongolo
Habari July 30, 2026
Wadau Wa Kilimo Iondoeni Nchi Kwenye Uchuuzi Wa Mafuta Ya Kula-Chongolo
Habari July 30, 2026
Mradi Wa Njia Ya Kusafirisha Umeme Wa Msongo Wa Kilovolti 400 Chalinze -Dodoma Mbioni Kukamilika
Habari July 29, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?